Kipengele cha sambaza kinakuruhusu kusambaza ujumbe kutoka katika soga ya binafsi au ya kikundi kwenda kwenye soga ya binafsi au kikundi kingine. Ujumbe uliosambazwa huashiriwa kwa lebo ya “Ulisambazwa” ambayo hukusaidia kujua kama rafiki au ndugu yako aliandika ujumbe aliotuma au ikiwa ujumbe huo ulitoka kwa mtu mwingine hapo awali.
Unaweza kusambaza hadi soga tano kwa wakati mmoja. Ujumbe unaposambazwa mara nyingi, unaweza tu kusambazwa kwa soga moja kwa wakati mmoja.
Sambaza ujumbe
Kwenye soga ya binafsi au ya kikundi, gusa na ushikilie ujumbe unaotaka kusambaza.
Kusambaza ujumbe kadhaa, unaweza kuchagua ujumbe zaidi baada ya kuchagua ujumbe wa kwanza.
Gusa Sambaza.
Tafuta au chagua soga za binafsi au za kikundi unazotaka kusambazia ujumbe.
Gusa Tuma.
Kumbuka:
Unaweza pia kusambaza media, mahali, au waasiliani ili usizipakie tena.
Ujumbe wowote unaosambaza ambao si wako mwenyewe utaonekana ukiwa na lebo ya "Ulisambazwa" kwako na kwa kila mpokeaji anayepata ujumbe huo.