Jinsi ya kuhariri picha na video
WhatsApp hukuruhusu kubadilisha unavyotaka picha na video zako kwa kuongeza emoji, maandishi au uchoraji kwa kidole.
Kuhariri picha na video
- Gusa
Kamera katika sehemu ya kuandikia. - Piga picha mpya au video, ama chagua picha au video iliyopo kwenye kichaguzi.
- Chagua unachotaka kuongeza kwenye picha au video.
Kuongeza vibandiko au emoji
- Gusa
Kibandiko > Kibandiko au Emoji. - Gusa kipengee ambacho ungependa kutumia.
- Ili usogeze kipengee, kiguse na ukishikilie, kisha kiburute.
- Ili ubadilishe ukubwa wa kipengee, kifinye au kipanue ili kiwe kidogo au kikubwa.
- Ili kuzungusha kipengee, kifinye na ukigeuze.
Kuongeza maandishi
- Gusa Maandishi
katika sehemu ya juu ya skrini. - Andika unachotaka katika sehemu ya maandishi.
- Ili uchague rangi, telezesha kidole chako juu na chini kwenye kiteua rangi.
- Ili uchague aina ya fonti, gusa Maandishi
kwa kurudia. Gusa skrini ili uthibitishe aina ya fonti. - Ili ubadilishe ukubwa wa maandishi, yafinye au yapanue ili yawe madogo au makubwa.
- Ili uzungushe maandishi, finya na ugeuze maandishi.
Kuchora
- Gusa
Chora katika sehemu ya juu ya skrini. - Tumia kidole chako kuchora unachotaka.
- Ili uchague rangi, telezesha kidole chako juu na chini kwenye kiteua rangi. Unaweza kuchagua rangi ya kila mstari unaouchora.
Kutumia vichujio
- Telezesha kidole juu kwenye picha au video.
- Chagua kichujio.
Kunyamazisha sauti ya video
- Gusa
Nyamazisha ili uondoe sauti kwenye video yako.