Unaweza kufuta jumbe kwako mwenyewe au omba kwamba jumbe zifutwe kwa kila mtu.
Futa jumbe kwa kila mtu
Kufuta jumbe kwa kila mtu kunakukubalia kufuta jumbe maalum ulizotuma kwa soga ya kibinafsi au kikundi. Hii ina faida ikiwa ulituma ujumbe kwa soga isiyo sawa au kama ujumbe uliotuma una makosa.
Jumbe ambazo zimefutwa tayari zitabadilishwa na:
“Ujumbe huu ulifutwa"
Kufuta jumbe za kila mtu:
Fungua WhatsApp na nenda kwenye soga iliyo na ujumbe unaotaka kufuta.
Gusa na shikilia ujumbe. Kwa hiari, chagua jumbe zaidi ili kufuta jumbe nyingi kwa mara moja.
Gusa Futa > Futa kwa kila mtu.
Kumbuka:
Ili jumbe zifutwe kwa ufanisi kwa kila mtu, wewe na mpokeaji wako lazima mtumie toleo la karibuni la WhatsApp.
Wapokeaji wanaotumia WhatsApp ya iOS bado wanaweza kuwa na media zilizotumwa kwenye Picha, hata baada ya kufutwa kwenye soga za WhatsApp.
Wapokeaji wanaweza kuona ujumbe kabla haujafutwa au kama ufutaji haukufanikiwa.
Hautaarifiwa kama ufutaji kwa kila mtu haukufanikiwa.
Una saa moja tu baada ya kutuma ujumbe kuuliza kutimiza Futa kwa kila Mtu.
Kujifutia jumbe
Unaweza kufuta nakili ya jumbe zako ulizotuma au kupokea kwa simu yako. Hii haina athari kwenye soga za wapokeaji wako. Wapokeaji wako bado wataona jumbe katika skrini zao za soga.
Kujifutia jumbe:
Fungua WhatsApp na nenda kwenye soga iliyo na ujumbe ungetaka kufuta.
Gusa na shikilia ujumbe. Kwa hiari, gusa jumbe zaidi ili kufuta jumbe nyingi kwa mara moja.