Jinsi ya kuunda na kualika washiriki kwenye kikundi
Unaweza kuunda kikundi cha WhatsApp chenye hadi washiriki 256.
Kuunda kikundi
Fungua WhatsApp > gusa Chaguo zaidi > Kikundi kipya.
Au, gusa Soga mpya > Kikundi kipya.
Tafuta au chagua waasiliani wa kuongeza kwenye kikundi. Kisha, gusa aikoni ya mshale wa kijani.
Weka mada ya kikundi. Hili litakua jina la kikundi ambalo washiriki wote wataliona.
Ukomo wa mada ni herufi 25.
Unaweza kugusa Emoji ili uweke emoji kwenye mada yako.
Unaweza kuweka aikoni ya kikundi kwa kugusa aikoni ya Kamera. Unaweza kuchagua kutumia Kamera, Matunzio au Tafuta Mtandaoni ili uongeze picha. Ukishaweka, aikoni itaonekana karibu na kikundi kwenye kichupo cha SOGA.
Gusa aikoni ya tiki ya kijani unapomaliza.
Kualika washiriki kwenye vikundi kupitia viungo
Ukiwa msimamizi wa kikundi, unaweza kuwaalika watu kujiunga na kikundi kwa kushiriki kiungo nao. Msimamizi anaweza Kubadilisha kiungo wakati wowote ili kubatilisha kiungo cha mwaliko wa awali na kuunda kiungo kipya.
Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA. Kisha, gusa Chaguo zaidi > Maelezo ya kikundi.
Gusa Alika kupitia kiungo.
Chagua Kutuma kiungo kupitia WhatsApp, Nakili kiungo, Kushiriki kiungo kupitia programu nyingine, au msimbo wa QR.
Ikiwa unatuma kupitia WhatsApp, tafuta au uchague waasiliani, kisha uguse Tuma.
Ili ubadilishe kiungo, gusa Badilisha kiungo > BADILISHA KIUNGO.
Kumbuka: Mtumiaji yeyote wa WhatsApp unayeshiriki naye kiungo anaweza kujiunga na kikundi, kwa hiyo tumia kipengele hiki na watu unaowaamini tu. Inawezekana mtu akasambaza kiungo kwa watu wengine, ambao wanaweza kujiunga na kikundi bila kuwa na ruhusa ya ziada kutoka kwa msimamizi wa kikundi.