Jinsi ya kufuta soga
Kufuta soga kunakuruhusu kufuta jumbe zote ndani ya soga. Soga bado itaorodheshwa kwenye orodha ya soga.
Kufuta soga ya kibinafsi au kikundi
- Kwenye tab ya Soga, fungua soga ya kibinafsi au ya kikundi unayotaka kufuta.
- Gusa Hiari zaidi
> Zaidi > Futa soga. - Chagua au usichague Futa jumbe zilizo na nyota na Futa media kwenye soga hii.
- Gusa FUTA.
Futa soga zote kwa wakati mmoja
- Kwenye tab ya Soga, gusa Hiari zaidi
> Mipangilio > Soga > Historia ya soga. - Gusa Kuondoa soga zote
- Chagua au usichague Futa jumbe zilizo na nyota na Futa media kwenye soga.
- Gusa FUTA JUMBE.