Jinsi ya kuweka au kutoa soga au kikundi nyarakani
Kipengele cha kunyarakisha kinakuruhusu kuficha soga za binafsi au za kikundi kutoka kwenye orodha yako ya soga ili kupangilia mazungumzo yako vizuri.
Kumbuka:
- Kunyarakisha soga hakutafuta au kuhifadhi nakala ya soga kwenye kadi yako ya SD.
- Soga binafsi au za kikundi zilizonyarakishwa zitabakia nyarakani utakapopokea ujumbe mpya kutoka kwa mtu yuyo huyo au soga ya kikundi.
- Hutapokea arifa za soga zilizonyarakishwa isipokuwa kama umetajwa au kujibiwa.
Kunyarakisha soga ya binafsi au ya kikundi
- Kwenye kichupo cha SOGA, gusa na ushikilie soga unayotaka kuificha.
- Gusa
Zilizonyarakishwa juu ya skrini.
Kunyarakisha soga zote
- Kwenye kichupo cha SOGA, gusa Chaguo zaidi
> Mipangilio. - Gusa Soga > Historia ya soga > Nyarakisha soga zote.
Kuona soga za binafsi ua za kikundi zilizonyarakishwa
- Telezesha hadi juu ya skrini ya SOGA.
- Gusa
Zilizonyarakishwa.
Nambari iliyo karibu na
Kuondoa soga ya binafsi au ya kikundi nyarakani
- Telezesha hadi juu ya skrini ya SOGA.
- Gusa
Zilizonyarakishwa. - Gusa na ushikilie soga ya binafsi au ya kikundi unayotaka kuiondoa nyarakani.
- Gusa Toa nyarakani katika sehemu ya juu ya skrini.
Mipangilio mbadala ya kunyarakisha
Kubadilisha mipangilio ya kawaida ili soga zilizonyarakishwa zitoke nyarakani ujumbe mpya unapopokelewa na kuondoa
- Kwenye kichupo cha SOGA, gusa Chaguo zaidi
> Mipangilio - Gusa Soga.
- Zima Soga zibakie nyarakani.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kunyarakisha au kutoa soga au kikundi nyarakani: iPhone | Web na Desktop | KaiOS