Kipengele cha kunyarakisha kinakuruhusu kuficha soga za kibinafsi au kikundi kutoka kwa orodha ya soga zako ili kupangilia mazungumzo yako.
Kumbuka:
- Kutumia nyarakisha hakutafuta au kucheleza soga kwenye kadi yako ya SD.
- Soga ya kibinafsi au kikundi iliyonyarakishwa itatolewa nyarakani utakapo pokea ujumbe mpya kutoka kwa huyo mtu binafsi au soga ya kikundi.
Nyarakisha soga au kikundi
- Kwenye tab ya SOGA, gusa na shikilia soga unayotaka kuficha.
- Gusa Nyarakisha
juu ya skrini.
Nyarakisha soga zote
- Kwenye tab ya SOGA, gusa Hiari zaidi
> Mipangilio. - Gusa Soga > Historia ya soga > Nyarakisha soga zote.
Tazama soga au vikundi vilivonyarakishwa
- Sogeza mpaka chini ya skrini ya SOGA.
- Gusa Imenyarakishwa.
Kutoa nyarakani soga au kikundi
- Sogeza mpaka chini ya skrini ya SOGA na gusa Nyarakisha.
- Gusa na shikilia soga au kikundi unayotaka kutoa nyarakani.
- Kwenye kibao cha juu, gusa ikoni ya kutoa nyarakani.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kunyarakisha au kutoa nyarakani soga au kikundi: iPhone | | Web na Desktop | KaiOS