Jinsi ya kutumia hali ya giza
Hali ya giza inakuruhusu kubadilisha rangi ya mandhari ya WhatsApp kutoka nyeupe hadi nyeusi.
Tumia hali ya giza
- Fungua WhatsApp, kisha gusa Hiari zaidi > Mipangilio > Soga > Mandhari.
- Chagua kutoka kwenye hiari zifuatazo:
- Giza: Washa hali ya giza.
- Nuru: Zima hali ya giza.
- Mfumo msingi: Wezesha mandhari ya giza ya WhatsApp ili ifanane na mipangilio ya kifaa chako. Nenda kwa kifaa Mipangilio > Uonyesho > washa au zima Mandhari ya giza.