Jinsi ya kuongeza hifadhi kwenye WhatsApp
Unaweza kuangalia ni kiasi gani cha nafasi kinachukuliwa na WhatsApp kwenye kifaa chako na kuongeza nafasi kwa kufuta vipengee.
Tazama hifadhi
- Kwenye SOGA gusa, gusa Hiari zaidi
> Mipangilio. - Gusa Hifadhi na data > Dhibiti hifadhi.
Kiasi cha nafasi kinachotumiwa kwenye kifaa chako na Midia ya WhatsApp na Programu na vipengee vingine vinaonyeshwa juu ya skrini.
Kagua na futa vipengee
Unaweza kuongeza nafasi kwa kufuta vipengee ambavyo ni vikubwa au vimesambazwa mara nyingi. Unaweza pia kufuta vipengee kwa kila soga.
Kukagua vipengee
- Kwenye SOGA gusa, gusa Hiari zaidi
> Mipangilio. - Gusa Hifadhi na data > Dhibiti hifadhi.
- Gusa Ilisambazwa mara nyingi, Kubwa zaidi ya MB 5 au chagua soga maalumu.
- Unaweza kugusa aikoni ya kupanga ili upange kwa Mpya kabisa, Zamani zaidi, au Kubwa zaidi.
- Ukubwa wa faili wa vipengee unaonyeshwa kwenye kona ya juu ya kipengee.
- Gusa kipengee kukikagua. Unaweza pia:
- Angalia ni soga gani kipengee hicho kinapotoka na ilipotumwa: Gusa Zaidi
> Onyesha kwenye soga. - Weka nyota au ondoa nyota kwenye kipengee: Gusa Nyota
au Ondoa nyota .
Kufuta vipengee
Ukichagua kufuta kipengee, kitafutwa kutoka kwa midia yako ya WhatsApp. Vipengee vilivyofutwa bado vinaweza kuhifadhiwa kwenye kifaa chako. Kama una nakala kadhaa za kipengee, utahitajika pia kufuta nakala zote ili kuongeza nafasi.
- Kwenye SOGA gusa, gusa Hiari zaidi
> Mipangilio. - Gusa Hifadhi na data > Dhibiti hifadhi.
- Gusa Ilisambazwa mara nyingi, Kubwa zaidi ya MB 5 au chagua soga maalumu.
- Unaweza:
- Kuchagua vipengee vyote: Gusa Chagua Vyote kama unataka kufuta vipengee vyote kwa mara moja.
- Kufuta vipengee binafsi: Gusa na shikilia kipengee unachotaka kukifuta. Chagua vipengee vingine vya kufuta ili kufuta vipengee vingi mara moja.
- Gusa Futa
. - Chagua Futa vipengee vyenye nyota kufuta vipengee vyenye nyota.
- Chagua Futa nakala zozote kufuta nakala rudufu.
- Gusa FUTA.
Kufuta vipengee kwa kuvitafuta
Unaweza pia kufuta vipengee binafsi kwa kutumia kipengele cha utafutaji.
- Kwenye SOGA gusa, gusa Tafuta
. - Gusa Picha, Video, au Nyaraka.
- Gusa kipengee unachotaka kukifuta.
- Gusa Zaidi
> Futa. - Mbadala, gusa Futa midia kwenye soga hii.
- Gusa FUTA.
Arifa za hifadhi ndogo
Ikiwa kiasi cha nafasi iliyopo kwenye kifaa chako kinafikia kiasi cha chini sana, WhatsApp huenda isiweze kufanya kazi vizuri. Kama hili likitokea, WhatsApp inaweza kukuuliza uongeze nafasi ili uendelee kutumia programu hii.
Unaweza pia kuongeza nafasi kwa kufuta programu usizotumia au video kubwa, picha au faili zilizohifadhiwa kwenye simu yako. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuongeza nafasi kwenye simu yako nje ya WhatsApp, tafadhali wasiliana na mtengenezaji wa simu yako.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kuongeza nafasi kwenye WhatsApp kwa iPhone
- Kuhusu kikomo cha kusambaza