Jinsi ya kuhariri jalada lako
Unaweza kuhariri picha yako ya jalada, jina na taarifa kuhusu kwenye mipangilio ya WhatsApp.
Hariri picha yako ya jalada
- Fungua WhatsApp > gusa Hiari zaidi
> Mipangilio. - Gusa picha yako ya jalada.
- Gusa Matunzio kuchagua picha iliyopo au Kamera
kupiga picha mpya. - Kama una picha iliyopo sasa unaweza kuondoa picha.
Hariri jina lako la jalada
- Fungua WhatsApp > gusa Hiari zaidi
> Mipangilio. - Gusa picha yako ya jalada.
- Kwa Jina, gusa Hariri
. - Ingiza jina lako jipya.
- Kikomo cha jina ni herufi 25.
- Unaweza kuongeza emoji kwa kugusa Emoji
.
- Gusa HIFADHI.
Jina lako la jalada litaonekana kwa watumiaji kwenye vikundi ambavyo hawajahifadhi maelezo yako ya mawasiliano kwenye vitabu vya anwani zao.
Hariri taarifa za kukuhusu
- Fungua WhatsApp > gusa Hiari zaidi
> Mipangilio. - Gusa picha yako ya jalada.
- Kwa Kuhusu, gusa Hariri
. - Unaweza kufanya mojawapo:
- Chagua picha ya jalada.
- Gusa Hariri
kwa Sasa imewekwa kwa kubinafsisha taarifa zako. Kikomo cha maelezo ni herufi 139.
Taarifa zako haziwezi kuwa tupu.
Dokezo:
- Unaweza kubadilisha mipangilio yako ya faragha ili kudhibiti nani anayeweza kuona picha ya jalada lako au taarifa kukuhusu.
- Unaweza kuamua nani anayeweza kukuongeza kwenye vikundi kwa kubadilisha mipangilio yako ya faragha ya kikundi.
- Kama ukimzuia mwasiliani, huyo mtu hataona sasisho zozote za picha ya jalada yako au taarifa.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kuhariri jalada lako kwenye: iPhone | Web na Desktop | KaiOS
- Jinsi ya kubadilisha mipangilio yako ya faragha
- Jinsi ya kubadilisha mipangilio yako ya faragha za kikundi