Unaweza kuifuta akaunti yako ndani ya WhatsApp. Kufuta akaunti yako ni mchakato usioweza kurekebishwa, ambao hatuwezi kurejesha hata kama umeifanya kimakosa.
Chagua sababu ya kufuta akaunti kutoka kwa kijunzi.
Gusa FUTA AKAUNTI YANGU.
Kuifuta akaunti yako kutafanya yafuatayo:
Kutafuta akaunti yako kutoka kwa WhatsApp.
Kutafuta historia yako ya ujumbe.
Kutakufuta kutoka kwa vikundi vyako vyote vya WhatsApp.
Kutafuta chelezo lako la Google Drive.
Ukiifuta akaunti yako:
Huwezi kurejesha ufikiaji wa akaunti yako.
Inaweza kuchukua hadi siku 90 kutoka mwanzo wa mchakato wa kufuta ili kufuta maelezo yako ya WhatsApp. Nakala za maelezo yako huenda pia zikabaki baada ya siku 90 kwenye hifadhi ya chelezo tunayotumia ili kurejesha katika tukio la mkasa, kosa la programu au tukio lingine la kupoteza data. Maelezo yako hayapatikani kwako kwenye WhatsApp kwa wakati huu.
Haiathiri maelezo ya watumiaji wengine wanaohusiana na wewe, kama vile nakala zao za ujumbe ulizowatumia.
Nakala za nyenzo kama vile nakili za kumbukumbu zinaweza kubaki katika hifadhidata yetu lakini zimetengwa na vitambulisho vya kibinafsi.
Tunaweza pia kuweka taarifa zako kwa mambo kama masuala ya kisheria, ukiukaji wa masharti, au juhudi za kuzuia madhara.
Tafadhali rejea sehemu ya Sheria na Ulinzi ya Sera yetu ya Faragha kwa maelezo zaidi.