WhatsApp inatambua kwa haraka na kwa urahisi ni nani kati ya waasiliani wako wanaotumia WhatsApp kwa kupitia kitabu cha anwani ya simu yako.
Kuongeza mwasiliani mpya
- Hifadhi jina na namba ya simu ya mwasiliani kwenye kitabu cha anwani ya simu yako.
- Kama ni namba ya eneo lako: Hifadhi namba kwa katika muundo sawa unayoweza kutumia ikiwa ungepiga simu hiyo.
- Ikiwa ni namba ya kigeni: Hifadhi namba katika muundo wa kimataifa kamilifu:
- + [Msimbo wa Nchi] [Namba Kamilifu ya Simu].
- Acha 0 yoyote inayoongoza kutoka kwa namba.
- Fungua WhatsApp na nenda kwenye tab ya Soga.
- Gusa ikoni ya soga mpya
ikoni > Hiari zaidi
> Changamsha.
Utatuaji
Ikiwa hawaoni waasiliani wako:
- Hakikisha umeruhusu WhatsApp kuingia kwenye waasiliani waliopo kwenye Mipangilio ya programu ya simu yako.
- Kwenye kitabu cha anwani cha simu yako, hakikisha akaunti na vikundi vyote vimewekwa kuwa “onekana” au “tazamwa”.
Jifunze jinsi ya kumuongeza mwasiliani kwenye: iPhone | Windows Phone