Jinsi ya kutafuta kwenye intaneti ujumbe wa WhatsApp uliosambazwa

Ukipokea ujumbe ambao umesambazwa kutoka kwa mtumiaji mmoja hadi kwa mwingine mara nyingi, unaweza kuanzisha utafutaji kwenye intaneti kutoka katika soga ya WhatsApp ili upate taarifa inayohusiana na yaliyo kwenye ujumbe. Ujumbe kama huo huashiriwa kwa aikoni ya vishale viwili
. Kipengele hiki kinapatikana kwa watumiaji nchini Ajentina, Brazili, Chile, Kolombia, Jamhuri ya Dominika, Ufaransa, Ujerumani, Ayalandi, Italia, Meksiko, Naijeria, Peruu, Uhispania, Uingereza, Marekani na Venezuela.
Kumbuka: Ukichagua kutafuta maudhui ya ujumbe kwenye wavuti, kipengele hiki kitakuruhusu kupakia maudhui ya ujumbe moja kwa moja kwenye Google bila ya kuyashiriki na WhatsApp. Masharti ya Google ya Huduma na Sera ya Faragha yatatumika.
  1. Gusa Tafuta
    karibu na ujumbe uliosambazwa.
  2. Gusa Tafuta kwenye Wavuti.
  3. Utafutaji utakuelekeza kwenye kivinjari cha wavuti ambapo matokeo yako yataonyeshwa kwenye Google.
Rasilimali Zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La