Jinsi ya kusambaza ujumbe

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Tumia kipengele cha kusambaza ili usambaze ujumbe kutoka kwenye soga ya binafsi au ya kikundi kwenda kwenye soga nyingine ya binafsi au ya kikundi. Ujumbe uliosambazwa huashiriwa kwa lebo “Umesambazwa”, ili kukusaidia kujua kama rafiki au ndugu yako aliandika ujumbe aliotuma au ikiwa ujumbe huo ulitoka kwa mtu mwingine hapo awali.
Unaposambaza ujumbe, unaweza kuushiriki kwenye hadi soga tano kwa wakati mmoja. Ikiwa ujumbe tayari umesambazwa, unaweza kuusambaza kwenye hadi soga tano, ikiwa ni pamoja na kwenye soga moja ya kikundi. Ujumbe ukiwa umesambazwa mara nyingi, unaweza tu kusambazwa kwenda kwenye soga moja kwa wakati.

Kusambaza ujumbe
 1. Kwenye soga ya mtu binafsi au ya kikundi, wekelea kiashiria kwenye ujumbe unaotaka kuusambaza, kisha ubofye Menyu
  > Sambaza ujumbe.
  • Ili kusambaza ujumbe mwingi, unaweza kuchagua ujumbe wa ziada baada ya kuchagua ujumbe wa kwanza au ubofye Menyu (
   au
   ) > Chagua ujumbe > kuchagua ujumbe unaotaka kusambaza.
 2. Bofya Sambaza ujumbe (
  au
  ).
 3. Tafuta au chagua soga za binafsi au za kikundi unazotaka kuzisambazia ujumbe.
 4. Bofya Tuma (
  au
  ).
Kumbuka: Ujumbe wowote unaousambaza ambao si ujumbe wako mwenyewe unaotuma utaonyesha lebo "Umesambazwa" kwako na kwa mpokeaji yeyote atakayepokea ujumbe huo.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La