Jinsi ya kusambaza ujumbe

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Tumia kipengele cha kusambaza ili usambaze ujumbe kutoka kwenye soga ya binafsi au ya kikundi kwenda kwenye soga nyingine ya binafsi au ya kikundi. Ujumbe uliosambazwa huashiriwa kwa lebo “Ulisambazwa” ili kukusaidia kujua kama rafiki au ndugu yako aliandika ujumbe aliotuma au ikiwa ujumbe huo ulitoka kwa mtu mwingine hapo awali.
Unaposambaza ujumbe, unaweza kuushiriki kwenye hadi soga tano kwa wakati mmoja. Ikiwa ujumbe tayari umesambazwa, unaweza kuusambaza kwenye hadi soga tano, ikiwa ni pamoja na kwenye soga moja ya kikundi. Ujumbe ukiwa umesambazwa mara nyingi, unaweza tu kusambazwa kwenda kwenye soga moja kwa wakati.
Kusambaza ujumbe
  1. Kwenye soga ya binafsi au ya kikundi, chagua ujumbe unaotaka kuusambaza.
  2. Bonyeza Chaguo > Sambaza.
  3. Tafuta au chagua mtu au kikundi unachotaka kukisambazia ujumbe > ONGEZA.
  4. Bonyeza Nimemaliza.
Kumbuka:
  • Maelezo mafupi hayatasambazwa pamoja na maudhui.
  • Ujumbe wowote unaousambaza ambao si ujumbe wako unaotuma utakuwa na maneno “Ulisambazwa” kwako na kwa kila mpokeaji anayepata ujumbe huo.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La