Jinsi ya kusambaza ujumbe

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Kipengele cha sambaza kinakuruhusu kusambaza ujumbe kutoka katika soga ya binafsi au ya kikundi kwenda kwenye soga nyingine ya binafsi au ya kikundi. Ujumbe uliosambazwa huashiriwa kwa lebo ya “Ulisambazwa” ili kukusaidia kujua kama rafiki au ndugu yako aliandika ujumbe aliotuma au ikiwa ujumbe huo ulitoka kwa mtu mwingine hapo awali.
Unaweza kusambaza ujumbe kwenye hadi soga tano kwa wakati mmoja. Ikiwa ujumbe tayari umesambazwa, unaweza kuusambaza kwenye hadi soga tano, ikiwa ni pamoja na kwenye soga moja ya kikundi. Ujumbe ukiwa umesambazwa mara nyingi, unaweza tu kusambazwa katika soga moja kwa wakati.

Kusambaza ujumbe
 1. Kwenye soga ya binafsi au ya kikundi, gusa na ushikilie ujumbe unaotaka kuusambaza.
  • Kusambaza ujumbe kadhaa, unaweza kuchagua ujumbe zaidi baada ya kuchagua ujumbe wa kwanza.
 2. Gusa Sambaza
  .
 3. Tafuta au chagua soga za binafsi au za kikundi unazotaka kuzisambazia ujumbe.
 4. Gusa Tuma
  .
Kumbuka:
 • Unaweza pia kusambaza maudhui, mahali au anwani ili usiwe na ulazima wa kuzipakia tena.
 • Ujumbe wowote unaosambaza ambao si ujumbe wako unaotuma utakuwa na maneno "Ulisambazwa" kwako na kwa kila mpokeaji anayepata ujumbe huo.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La