Kuhusu kujiunga na kujiondoa kwenye soga za biashara

WhatsApp inataka uwe na udhibiti wa nani anayepiga soga nawe. Hii ndiyo sababu biashara haiwezi kuendelea kuwa na mazungumzo nawe isipokuwa kama umechagua kupiga soga na biashara husika.
Biashara inapokutumia ujumbe kwa mara ya kwanza, utakuwa na aina tatu ya mitagusano ya kuchagua. Gusa:
  • Zuia ili uongeze biashara kwenye orodha yako ya Anwani ulizozuia. Unapozuia biashara, biashara husika haitaweza kukutumia ujumbe moja kwa moja. Hata hivyo, bado utaweza kufikia jalada na katalogi ya biashara husika. Pia, utaweza kuwasiliana na biashara husika ikiwa mpo katika kikundi chochote kwa pamoja.
  • Ripoti kuripoti biashara ikiwa unafikiri inakiuka Sera yetu ya Uuzaji. Unaweza pia kutumia chaguo hili kuzuia biashara.
  • Endelea ili uendelee kupiga soga na biashara. Unaweza pia kuchagua kujiunga kwa kutuma ujumbe kwa biashara.
Kujiondoa kwenye ujumbe wa mauzo kutoka kwa biashara
Baadhi ya biashara zinaweza kutoa chaguo la kujiondoa katika kupokea ujumbe wa mauzo kwa kugusa kitufe cha Kujiondoa kwenye ujumbe wa mauzo katika soga zako za biashara (maandishi kamili kwenye kitufe yanaweza kutofautiana). Kugusa kitufe hiki kutaarifu biashara kuwa ungependa kuondoa namba yako ya WhatsApp kwenye orodha ya biashara hiyo ya wanaopokea ujumbe wa mauzo. Huenda biashara zikajiondolea namba yako kwenye orodha ya watu wanaopokea ujumbe wao, kwa hivyo kunaweza kuwa na kuchelewa kati ya unapojiondoa na unapoacha kupokea ujumbe wa mauzo.
Biashara zinaweza kukuomba kutoa sababu ya kujiondoa; unaweza kuchagua kutotoa sababu. Kwa njia hii biashara inaweza kujifunza kupitia maoni yako na kuhakikisha kuwa ujumbe husika unafaa kwa wateja wao. Pia, zinapokutumia ujumbe wa uthibitisho wa kujiondoa, baadhi ya biashara zinaweza kujumuisha chaguo la kujijumuisha kwenye kupokea ujumbe wa mauzo ikiwa umebadili mawazo au ikiwa ulijiondoa kimakosa.
Kujiondoa kwenye ujumbe wa mauzo kukilinganishwa na kuzuia biashara
Ingawa kuzuia biashara husitisha biashara kukutumia ujumbe, pia hukusitisha kuweza kutumia biashara hiyo ujumbe. Kutumia kitufe cha Kujiondoa kwenye ujumbe wa mauzo hutuma ombi la kujiondoa kwenye orodha ya ujumbe wa mauzo ya biashara husika, lakini bado kunaruhusu ujumbe wa binafsi kati yako na biashara kuendelea. Kwa njia hii, bado unaweza kuwasiliana na biashara ukiwa na maswali kuhusu bidhaa au huduma husika na biashara zinaweza kukutumia ujumbe unaohusiana na miamala yako kama vile arifa kuhusu usafirishaji.
Rasilimali zinazohusiana
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La