Jinsi ya kutumia orodha ya matangazo

Android
iPhone
Tumia kipengele cha orodha ya matangazo ili kutuma ujumbe kwa anwani zako kadhaa kwa wakati mmoja. Orodha ya matangazo ni orodha za anwani zinazohifadhiwa ambazo unaweza kutuma ujumbe mara kwa mara bila kuzichagua kila wakati.
Kuunda orodha ya matangazo
  1. Gusa Soga > Orodha ya Matangazo > Orodha Mpya.
  2. Tafuta au chagua anwani unazotaka kuziongeza.
  3. Gusa Unda.
Wapokeaji hupokea ujumbe kutoka kwenye orodha yako ya matangazo kama ujumbe wa kawaida katika kichupo chao cha Soga. Majibu yao pia yataonekana kama ujumbe wa kawaida na hayatatumwa kwa anwani zingine kwenye orodha ya matangazo.
Kumbuka: Watu ambao wamekuhifadhi kwenye orodha ya anwani kwenye simu zao pekee ndio watakaopokea ujumbe wako wa matangazo. Ikiwa mtu hapokei ujumbe wako wa matangazo, hakikisha kuwa amekuhifadhi kwenye orodha yake ya anwani. Orodha ya matangazo ni njia ya mawasiliano kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa watu wengi. Ukitaka wapokeaji wako washiriki kwenye mazungumzo ya kikundi, unapaswa kuunda soga ya kikundi badala yake.
Kuhariri orodha ya matangazo
  1. Fungua Orodha ya Matangazo yako.
  2. Gusa aikoni ya "i" iliyo karibu na orodha unayotaka kuhariri.
  3. Kwenye skrini ya Maelezo ya Orodha, unaweza:
    • Kubadilisha jina la orodha yako ya matangazo.
    • Kuongeza au kuondoa wapokeaji kwenye orodha kwa kugusa Hariri orodha....
Kufuta orodha ya matangazo
  1. Gusa Soga > Orodha ya Matangazo.
  2. Telezesha kushoto kwenye orodha ya matangazo unayotaka kufuta.
  3. Gusa Futa.
Au gusa Hariri, kisha aikoni ya "–" iliyo karibu na orodha unayotaka kufuta > Futa.
Rasilimali Zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La