Â
Jinsi ya kutumia orodha ya tangazo
Android
iPhone
Kwa kipengele cha orodha ya tangazo unaweza kutuma ujumbe kwa waasiliani wako kadhaa kwa mara moja. Orodha za tangazo ni orodha zilizohifadhiwa za wapokeaji wa ujumbe ambao unaweza kuwatumia mara kwa mara tangazo za jumbe bila kuwachagua kila mara.
Unda orodha ya tangazo
- Nenda kwa WhatsApp > Hiari zaidi> Tangazo jipya.
- Tafuta au chagua waasiliani unaotaka kuwaongeza.
- Gusa alama za uhakiki.
Hii itaunda orodha mpya ya tangazo. Unapotuma ujumbe kwa orodha ya tangazo, itatuma kwa wapokeaji wote ambao wamehifadhi namba yako kwenye vitabu vya anwani kwenye simu zao. Wapokeaji watapokea ujumbe kama ujumbe wa kawaida. Wakijibu ujumbe utaonekana kama ujumbe wa kawaida kwenye skrini yako ya SOGA. Majibu yao hayatatumwa kwa wapokeaji wengine kwenye orodha ya tangazo.
Kumbuka: Waasiliani tu waliokuongeza kwenye kitabu cha anwani cha simu zao watapokea ujumbe wako wa tangazo. Ikiwa mwasiliani wako hapokei jumbe za matangazo yako, angalia kuhakikisha kuwa wamekuongeza kwenye vitabu vyao vya anwani. Orodha za tangazo ni mawasiliano ya moja-kwa-wengi. Ukitaka wapokeaji washiriki kwenye mazungumzo ya kikundi, unapaswa kuunda soga ya kikundi badala yake.
Hariri orodha ya tangazo
- Fungua orodha yako ya tangazo.
- Gusa Hiari zaidi> Maelezo ya orodha ya tangazo.
- Kwenye skrini ya maelezo ya orodha ya tangazo unaweza:
- Badilisha jina la orodha ya tangazo kwa kugusa Hariri.
- Ongeza wapokeaji kwenye orodha kwa kugusa Ongeza mwasiliani....
- Ondoa mpokeaji kwa kugusa Hariri mpokeaji > "x" karibu na mwasiliani unayetaka kumuondoa > alama za uhakiki.
- Badilisha jina la orodha ya tangazo kwa kugusa Hariri
Futa orodha ya tangazo
- Gusa na shikilia orodha ya tangazo unalotaka kufuta.
- Gusa Futa orodha ya tangazo> FUTA. Unaweza kuchagua kufuta media au hapana.
Mbadala, fungua orodha ya tangazo unalotaka kufuta, kisha gusa jina la orodha ya tangazo au mpokeaji > Orodha ya tangazo > FUTA.