Jinsi ya kutumia orodha ya matangazo

Android
iPhone
Tumia kipengele cha orodha ya matangazo ili kutuma ujumbe kwa anwani zako kadhaa kwa wakati mmoja. Orodha ya matangazo ni orodha za anwani zinazohifadhiwa ambazo unaweza kutuma ujumbe mara kwa mara bila kuzichagua kila wakati.
Kuunda orodha ya matangazo
 1. Gusa Chaguo zaidi
  > Tangazo jipya.
 2. Tafuta au chagua anwani unazotaka kuziongeza.
 3. Gusa
  .
Wapokeaji hupokea ujumbe kutoka kwenye orodha yako ya matangazo kama ujumbe wa kawaida katika kichupo chao cha Soga. Majibu yao pia yataonekana kama ujumbe wa kawaida na hayatatumwa kwa anwani zingine kwenye orodha ya matangazo.
Kumbuka: Watu ambao wamekuhifadhi kwenye orodha ya anwani kwenye simu zao pekee ndio watakaopokea ujumbe wako wa matangazo. Ikiwa mtu hapokei ujumbe wako wa matangazo, hakikisha kuwa amekuhifadhi kwenye orodha yake ya anwani. Orodha ya matangazo ni njia ya mawasiliano kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa watu wengi. Ukitaka wapokeaji wako washiriki kwenye mazungumzo ya kikundi, unapaswa kuunda soga ya kikundi badala yake.
Kuhariri orodha ya matangazo
 1. Fungua orodha yako ya matangazo.
 2. Gusa Chaguo zaidi
  > Maelezo ya orodha ya matangazo.
 3. Kwenye skrini ya maelezo ya orodha ya matangazo unaweza:
  • Kubadilisha jina la orodha yako ya matangazo kwa kugusa
   > Badilisha jina la orodha ya matangazo.
  • Kuongeza wapokeaji kwenye orodha ya matangazo kwa kugusa
   > Ongeza mpokeaji...
  • Kuondoa wapokeaji kwa kugusa Badilisha wapokeaji > "x" iliyo karibu na anwani unazotaka kuondoa >
   .
Kufuta orodha ya matangazo
 1. Gusa na ushikilie orodha ya matangazo unayotaka kufuta.
 2. Gusa
  > Futa. Unaweza kuchagua kufuta maudhui au la.
Rasilimali zinazohusiana
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La