Jinsi ya kuhariri jalada lako

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Kuhariri picha yako ya jalada
 1. Fungua WhatsApp > bofya aikoni ya picha yako ya jalada.
  • Au, bofya Menyu
   juu ya orodha ya soga zako > Mipangilio > picha ya jalada lako.
 2. Kama:
  • Una picha ya jalada: Fanya kiashiri chako kielee juu ya picha yako, kisha bofya BADILISHA PICHA YA JALADA, ambapo unaweza kuchagua Kuangalia picha, Kupiga picha, Kupakia picha, au Kuondoa picha.
  • Huna picha ya jalada: Bofya WEKA PICHA YA JALADA, ambapo unaweza kuchagua Kupiga picha au Kupakia picha.
Kuhariri jina la jalada lako
 1. Fungua WhatsApp > bofya aikoni ya picha yako ya jalada.
  • Au, bofya Menyu
   juu ya orodha ya soga zako > Mipangilio > picha ya jalada lako.
 2. Ili kusasisha jina la jalada lako, bofya Hariri
  .
  • Unaweza pia kuweka emoji kwa kubofya Emoji
   .
 3. Baada ya kumaliza kufanya mabadiliko, bofya alama ya tiki
  .
Kuhariri taarifa kukuhusu
 1. Fungua WhatsApp > bofya aikoni ya picha yako ya jalada.
  • Au, bofya Menyu
   juu ya orodha ya soga zako > Mipangilio > picha ya jalada lako.
 2. Kusasisha maelezo yalio kwenye "kuhusu", bofya Hariri
  .
  • Unaweza pia kuweka emoji kwa kubofya Emoji
   .
 3. Baada ya kumaliza kufanya mabadiliko, bofya alama ya tiki
  .
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kuhariri jalada lako: Android | iPhone | KaiOS
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La