Ikiwa imeshindwa kuunganisha kwenye WhatsApp

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Ikiwa huwezi kutuma au kupokea ujumbe kwenye WhatsApp, huenda huna muunganisho wa intaneti. Ili kuangalia muunganisho wa intaneti ya kifaa chako:
  • Angalia ikiwa kuna aikoni ya saa karibu na ujumbe wako badala ya alama ya tiki. Ikiwa ipo, ina maana kwamba ujumbe wako haujawasilishwa.
  • Angalia ishara ya mtandao kwenye kifaa chako ili uone ikiwa inamweka au haipo.
Utatuaji
Matatizo mengi ya muunganisho yanaweza kusuluhishwa kwa kufanya mojawapo ya yafuatayo:
Mipangilio ya kifaa
  • Anzisha upya kifaa chako kwa kukizima na kukiwasha tena.
  • Sasisha utumie toleo la hivi karibuni la WhatsApp linalopatikana kwenye Duka la Programu la Apple.
  • Fungua Mipangilio ya iPhone
    na uwashe kisha uzime Hali ya Ndege.
  • Fungua Mipangilio ya iPhone
    > gusa Data ya simu kisha uwashe Data ya Simu.
  • Fungua Mipangilio ya iPhone
    > gusa Wi-Fi na uwashe kisha uzime Wi-Fi.
  • Boresha au rejesha mfumo wa uendeshaji wa iPhone yako kuwa wa toleo la hivi karibuni kwa ajili ya kifaa chako.
Mipangilio ya Wi-Fi
  • Jaribu kuunganisha kwenye mitandao tofauti ya Wi-Fi.
  • Hakikisha unawasha Wi-Fi wakati unatumia hali ya Sleep Focus.
  • Zima kisha uwashe tena ruta yako ya Wi-Fi.
  • Wasiliana na kampuni inayokupa huduma za simu na uhakikishe mipangilio yako ya APN imewekwa kwa usahihi.
  • Fungua Mipangilio ya iPhone
    > gusa Jumla > Hamisha au Badilisha iPhone > Badilisha> Badilisha Mipangilio ya Mtandao. Weka msimbo wako wa siri. Chagua Badilisha Mipangilio ya Mtandao. (Kufanya hivi kutafuta manenosiri yako yote ya Wi-Fi uliyoyahifadhi).
  • Ikiwa unatatizika kuunganisha kwenye WhatsApp unapotumia mtandao wa Wi-Fi ambao kwa kawaida huwa hauutumii, wasiliana na msimamizi wa mtandao huo.
  • Hakikisha kuwa hutumii mtandao wa Wi-Fi unaodhibitiwa, kama vile ofisini au katika chuo kikuu. Inawezekana kwamba mtandao wako umewekwa mipangilio ili kuzuia au kupunguza miunganisho.
Mipangilio mingine
  • Ikiwa unatumia iPhone ambayo imefunguliwa au kadi ya SIM unayolipia awali, utahitaji kurekebisha mipangilio ya APN ya kifaa chako ili ifae kadi yako ya SIM. Wasiliana na kampuni inayokupa huduma za mtandao wa simu kwa maelezo na maelekezo.
  • WhatsApp haijaundwa ili kutumiwa kupitia seva mbadala au huduma za VPN. Mipangilio hiyo haiwezi kutumika.
  • Zima utumiaji wa mtandao wa ng'ambo.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La