Â
Jinsi ya kuongeza na kuondoa washiriki kwenye kikundi
Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kuwaongeza au kuwaondoa washiriki ikiwa wewe ni msimamizi wa kikundi.
Kuongeza washiriki
- Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubonyeze Chaguo > Ongeza washiriki.
- Au, chagua kikundi kwenye orodha ya soga zako. Kisha ubonyeze Chaguo > Maelezo ya Kikundi > Ongeza washiriki.
- Tafuta au chagua anwani unazotaka kuongeza kwenye kikundi.
- Bonyeza Nimemaliza.
Kuondoa washiriki
- Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubonyeze Chaguo > Maelezo ya kikundi.
- Au, chagua kikundi kwenye orodha ya soga zako. Kisha ubonyeze Chaguo > Maelezo ya Kikundi.
- Chagua mshiriki unayetaka kumwondoa.
- Bonyeza Chaguo > Mwondoe kwenye kikundi > ONDOA.