Â
Jinsi ya kuongeza na kuondoa washiriki
Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kuwaongeza au kuwaondoa washiriki ikiwa wewe ni msimamizi wa kikundi. Pia, wasimamizi wanaweza kuamua ikiwa wanataka kuweka vikundi vyao wazi ili mtu yeyote aliye kwenye WhatsApp ajiunge, au kuhitaji idhini ya msimamizi kwa washiriki wowote wapya wanaotaka kujiunga.
Kuongeza washiriki
- Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Au, telezesha kikundi kuelekea kushoto katika kichupo cha Soga. Kisha gusa Zaidi > Maelezo ya Kikundi.
- Gusa Ongeza Washirikiau Alika kwenye Kikundi kupitia Kiungo.
- Tafuta au chagua watumiaji unaotaka kuwaweka kwenye kikundi.
- Gusa Ongeza > Ongeza.
- Ikiwa kikundi kimewasha kipengele cha Kuidhinisha Washiriki Wapya na kuna maombi ya kujiunga kwenye kikundi yanayosubiri, msimamizi anaweza kukagua maombi haya.
Kuondoa washiriki
- Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
- Au, telezesha kikundi kuelekea kushoto katika kichupo cha Soga. Kisha gusa Zaidi > Maelezo ya Kikundi.
- Gusa mshiriki unayetaka kumwondoa.
- Gusa Ondoa kwenye Kikundi > Ondoa.
Rasilimali zinazohusiana: