Jinsi ya kuondoka kwenye akaunti

Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kuondoka katika akaunti kwenye vifaa vyote ukitumia simu yako kuu. Pia unaweza kuondoka moja kwa moja kwenye akaunti ya vifaa vyako vinavyofanya kazi pamoja kama vile WhatsApp Web, WhatsApp Desktop, simu nyinginezo ulizounganisha, kompyuta, kompyuta kibao za Android au Portal.
Kuondoka kwenye akaunti ya kompyuta yako
 1. Fungua WhatsApp Web au WhatsApp Desktop.
 2. Bofya Menyu (
  au
  ) juu ya orodha yako ya soga > Ondoka.
Kuondoka kwenye akaunti ukitumia simu yako kuu
 1. Fungua WhatsApp kwenye simu yako kuu.
  • Android: Gusa Chaguo zaidi
   > Vifaa vilivyounganishwa.
  • iPhone: Nenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp > gusa Vifaa Vilivyounganishwa.
 2. Gusa kifaa.
 3. Gusa ONDOA KWENYE AKAUNTI.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La