Jinsi ya kuunda na kudumisha katalogi

Android
iPhone
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Ili kuwapa wateja wako urahisi wa kufikia ofa mpya za biashara yako, endelea kusasisha katalogi yako.
Kuongeza bidhaa au huduma kwenye katalogi yako
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business > Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
  • Ikiwa unaanzisha bidhaa mpya, gusa Ongeza bidhaa mpya.
 2. Gusa Weka picha.
 3. Gusa Matunzio ili upakie picha kwenye kipengele chako cha Picha au Kamera ili kupiga picha mpya. Unaweza kupakia hadi picha 10.
 4. Weka jina la bidhaa au la huduma, pamoja na maelezo yoyote ya hiari kama vile:
  • Bei
  • Maelezo
  • Kiungo cha tovuti
  • Msimbo wa bidhaa au huduma
 5. Gusa HIFADHI.
Kumbuka: Kila picha iliyopakiwa kwenye katalogi itakaguliwa, ambayo itathibitisha kuwa picha, bidhaa au huduma inafuata Sera ya Uuzaji ya WhatsApp.
Bidhaa au huduma inapoidhinishwa, itaongezwa kiotomatiki kwenye katalogi. Hata hivyo, ikikataliwa, aikoni nyekundu ya mshangao itaonyeshwa karibu na picha.
Ikiwa unafikiri bidhaa yako ilikataliwa kimakosa, unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo:
 1. Gusa bidhaa iliyokataliwa.
 2. Gusa Omba ukaguzi mwingine.
 3. Weka sababu ya ombi lako.
 4. Gusa Endelea.
 5. Iwapo ulikagua Sera ya Uuzaji ya WhatsApp na rufaa yako ikakataliwa, tutumie jibu ukieleza ombi lako la ukaguzi wa tatu.
Kudhibiti bidhaa au huduma ambazo wateja wanaweza kutafuta
Kumbuka: Huenda bado usiweze kutumia kipengele hiki.
Kuficha bidhaa za katalogi
 1. Gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Zana za biashara > Katalogi.
 2. Unaweza kuficha bidhaa mojamoja au nyingi kwa pamoja.
  • Ili ufiche bidhaa moja, iguse ili ufungue ukurasa wa maelezo ya bidhaa hiyo. Kisha, uguse Chaguo zaidi
   > Ficha > Ficha.
  • Ili ufiche bidhaa kwa pamoja, bonyeza na ushikilie bidhaa hadi alama ya kijani ionekane. Kisha, uguse bidhaa nyingine unayotaka kuficha Ficha
   > Ficha.
  Kumbuka: Bidhaa ulizoficha bado zitaonekana kwenye kidhibiti chako cha katalogi zikiwa na
  juu ya picha ya bidhaa. Kwenye ukurasa wa maelezo ya bidhaa, kidokezo kinaonekana, kikionyesha kuwa umeficha kipengee hiki.
Kufichua bidhaa za katalogi
 1. Gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Zana za biashara > Katalogi.
 2. Unaweza kufichua bidhaa mojamoja au nyingi kwa pamoja.
  • Ili ufichue bidhaa moja, iguse ili ufungue ukurasa wa maelezo ya bidhaa hiyo. Kisha, uguse Chaguo zaidi
   > Fichua > Fichua.
  • Ili ufichue bidhaa kwa pamoja, bonyeza na ushikilie mojawapo ya bidhaa unayotaka kufichua mpaka alama ya kijani ionekane. Kisha, uguse bidhaa nyingine unazotaka kufichua > Fichua
   > Fichua.
Kufuta bidhaa au huduma kutoka kwenye katalogi yako
 1. Gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Zana za biashara > Katalogi.
 2. Bonyeza na ushikilie picha ya bidhaa au huduma.
 3. Gusa aikoni ya Futa, kisha uguse Futa.
Vinginevyo, chagua picha ya bidhaa au huduma unayotaka kuifuta. Kisha, gusa Chaguo zaidi
> Futa > Futa.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La