Kuhusu ufumbaji wa mwisho hadi mwisho

Faragha na usalama vipo kwenye damu yetu, ndiyo maana tumebuni ufumbaji wa mwisho hadi mwisho ndani ya programu yetu. Ufumbaji wa mwisho hadi mwisho ukiwepo, ujumbe wako, picha, video, ujumbe wa sauti, nyaraka, masasisho ya hali na simu hulindwa ili zisiingie kwenye mikono isiyofaa.
Utumaji ujumbe wa binafsi
Mfumo wa WhatsApp wa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho hutumika wakati wa soga kati yako na mtu mwingine anayetumia WhatsApp Messenger. Ufumbaji wa mwisho hadi mwisho huhakikisha kuwa ni wewe na mtu unayewasiliana naye pekee ndio mnaweza kusoma ujumbe au kusikiliza mawasiliano na kwamba hakuna mtu yeyote katikati, hata WhatsApp yenyewe. Hii ni kwa sababu kwa kutumia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, ujumbe wako hulindwa kwa kufuli, ni wewe na mpokeaji pekee ndio mlio na ufunguo maalum wa kuufungua na kusoma ujumbe huo. Haya yote hufanyika kiotomatiki: hutakiwi kuwasha mipangilio yoyote maalum ili kuhakikisha usalama wa ujumbe wako.
Utumaji ujumbe wa kibiashara
Kila ujumbe wa WhatsApp hulindwa na itifaki ile ile ya ufumbaji wa Ishara ambao hudumisha usalama wa ujumbe kabla haujatoka kwenye kifaa chako. Unapotuma ujumbe kwenda kwenye akaunti ya WhatsApp ya biashara, ujumbe wako hufikishwa kwa usalama kwenye sehemu iliyochaguliwa na biashara hiyo.
WhatsApp inachukulia kwamba soga kati yako na biashara zinazotumia programu ya WhatsApp Business au zinazosimamia na kujihifadhia ujumbe wa wateja huwa zimefumbwa mwisho hadi mwisho. Mara tu ujumbe ukishapokelewa, utakuwa chini ya taratibu za faragha za biashara husika. Biashara hiyo inaweza kuwapa idadi fulani ya wafanyakazi, au hata mashirika mengine, jukumu la kuchakata na kujibu ujumbe.
Baadhi ya biashara1 zitaweza kuchagua kampuni kuu ya WhatsApp, ambayo ni Meta, katika kuhifadhi ujumbe kwa usalama na kujibu wateja. Ingawa Meta haitatumia ujumbe wako moja kwa moja kubaini matangazo utakayoona, biashara zitaweza kutumia soga zinazopokea kwa madhumuni yao ya kimauzo, ambayo huenda yakajumuisha kutangaza kwenye Meta. Unaweza kuwasiliana na biashara husika wakati wowote ili upate maelezo zaidi kuhusu desturi zake za faragha.
Kumbuka: Hali ya ufumbaji wa mwisho hadi mwisho haiwezi kubadilika bila badiliko hilo kuonekana kwa mtumiaji. Kwa maelezo zaidi kuhusu ni soga zipi hufumbwa mwisho hadi mwisho, tafadhali soma waraka wetu rasmi.
Malipo
Malipo ya WhatsApp, ambayo yanapatikana kwenye nchi zilizochaguliwa, yanawezesha uhamishaji kati ya akaunti kwenye taasisi za kifedha. Kadi na namba za benki zinahifadhiwa zikiwa zimefumbwa kwenye mtandao wenye usalama sana. Hata hivyo, kwa kuwa taasisi za kifedha haziwezi kushughulikia miamala bila kupokea taarifa zinazohusiana na malipo haya, malipo haya hayafumbwi kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho.
Skrini ya "Thibitisha Msimbo wa Usalama" kwenye skrini ya maelezo ya mawasiliano ni nini?
Soga zinazofumbwa mwisho hadi mwisho kati yako na mtu mwingine zina msimbo wao wa usalama. Msimbo huu hutumika kuthibitisha kwamba simu na ujumbe unaotuma kwenye soga husika umefumbwa mwisho hadi mwisho.
Kumbuka: Mchakato wa uthibitishaji ni wa hiari kwa soga zilizofumbwa mwisho hadi mwisho na unatumiwa tu kuthibitisha kuwa ujumbe unaotuma na simu unazopiga zimefumbwa mwisho hadi mwisho.
Msimbo huu unapatikana kwenye skrini ya maelezo ya unayewasiliana naye, ukiwa msimbo wa QR pamoja na namba yenye tarakimu 60. Misimbo hii ni ya kipekee kwa kila soga binafsi na inaweza kulinganishwa kati ya watu katika kila soga ili kuthibitisha kwamba ujumbe huo unaotuma kwenye soga umefumbwa mwisho hadi mwisho. Misimbo ya usalama ni matoleo yanayoonekana ya funguo maalum zinazoshirikiwa kati yenu - na usiwe na wasiwasi, misimbo hii si funguo halisi, funguo hizo huwa siri kila wakati. Unapothibitisha kuwa soga imefumbwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, kufanya hivyo pia kunathibitisha kuwa orodha yako ya vifaa na vya unayewasiliana naye vilivyounganishwa vimesasishwa.
Ili uthibitishe kuwa soga imefumbwa mwisho hadi mwisho:
  1. Fungua soga.
  2. Gusa jina la unayewasiliana naye ili ufungue skrini ya maelezo ya anwani.
  3. Gusa Ufumbaji ili uone msimbo wa QR na namba yenye tarakimu 60.
    • Kumbuka: Kipengele hiki kinapatikana tu ikiwa unawasiliana na mtu katika soga iliyofumbwa mwisho hadi mwisho.
Ikiwa wewe na unayewasiliana naye mko karibu, mmoja wenu anaweza kuchanganua msimbo wa QR wa mwenzake au kuuangalia ili kulinganisha namba yenye tarakimu 60. Ukichanganua msimbo wa QR na msimbo huo uwe unalingana, alama ya kijani itaonekana. Kwa kuwa inalingana, unaweza kuwa na uhakika hakuna mtu anayeingilia kati ya ujumbe au simu zako.
Ikiwa wewe na unayewasiliana naye hamko karibu, unaweza kumtumia namba yenye tarakimu 60 kupitia mfumo mwingine. Mjulishe unayewasiliana naye kwamba mara tu apokeapo msimbo wako, anapaswa kuuandika na kisha kuulinganisha na namba yenye tarakimu 60 inayoonekana kwenye skrini ya maelezo ya anwani chini ya sehemu ya Ufumbaji. Kwa Android na iPhone, unaweza kutumia kitufe cha Shiriki kilicho katika skrini ya Thibitisha Msimbo wa Usalama kutuma namba yenye tarakimu 60 kupitia SMS, barua pepe, nk.
Ikiwa misimbo haifanani, inawezekana kuwa unachanganua msimbo wa mtu tofauti au namba tofauti ya simu. Ikiwa unayewasiliana naye amesakinisha upya WhatsApp hivi karibuni, amebadili simu au ameongeza au kuondoa kifaa kilichounganishwa, tunapendekeza ufanye upya msimbo kwa kumtumia ujumbe mpya na kisha kuuchanganua msimbo huo. Pata maelezo zaidi kuhusu kubadilisha misimbo ya usalama kwenye makala haya.
Tafadhali kumbuka, ikiwa wewe au unayewasiliana naye mnatumia WhatsApp kwenye vifaa vingi, utahitaji kuthibitisha msimbo wa usalama kwenye vifaa vyako vyote na vya unayewasiliana naye.
Kwa nini WhatsApp inatoa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho na ina maana gani kwa kuwaweka watu salama?
Usalama ni muhimu kwa huduma ambayo WhatsApp inayotoa. Tumeona mifano mingi ambapo wadukuzi wahalifu walipata kiasi kikubwa cha data za binafsi kinyume na sheria na kutumia vibaya teknolojia ili kuwaumiza watu na taarifa zao zilizoibiwa. Tangu tulipomaliza utekelezaji wa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho mwaka 2016, usalama dijitali umezidi kuwa muhimu.
WhatsApp haina uwezo wa kuona maudhui ya ujumbe au kusikiliza simu zilizofumbwa mwisho hadi mwisho. Hiyo ni kwa sababu ufumbaji na ufumbuaji wa ujumbe uliotumwa na kupokelewa kwenye WhatsApp hufanyika kikamilifu kwenye kifaa chako. Kabla ya ujumbe kuondoka kwenye kifaa chako, huwa umelindwa kwa kufuli la usimbaji, ni mpokeaji pekee ndiye ana funguo za ujumbe. Zaidi ya hayo, funguo hubadilika kwa kila ujumbe unaotumwa. Ingawa haya yote hufanyika chinichini, unaweza kuthibitisha kuwa mazungumzo yako yanalindwa kwa kuangalia uthibitisho wa msimbo wa usalama kwenye kifaa chako. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu utendaji huu kwenye waraka wetu rasmi.
Kwa kawaida, watu huuliza ufumbaji wa mwisho hadi mwisho una athari gani kwa utekelezaji wa sheria. WhatsApp inathamini kazi ambayo inafanywa na watekelezaji wa sheria katika kuwaweka watu salama kote duniani. Huwa tunahakiki umakini, kuthibitisha na kujibu maombi ya watekelezaji wa sheria kulingana na sheria na sera husika na tunatoa kipaumbele kwa maombi ya dharura. Kama sehemu ya jitihada zetu za elimu, tumechapisha taarifa kwa ajili ya watekelezaji wa sheria kuhusu taarifa chache tunazokusanya na jinsi wanavyoweza kuziomba kutoka kwa WhatsApp, unaweza kuzisoma hapa.
Kujifunza kuhusu usalama wako kwenye WhatsApp, tafadhali tembelea Usalama wa WhatsApp.
1Mwaka wa 2021.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La