Jinsi ya kuhariri picha na video

Android
iPhone
WhatsApp hukuruhusu kubadilisha unavyotaka picha na video zako kwa kuongeza emoji, maandishi au uchoraji kwa kidole.
Kuhariri picha na video
 1. Gusa
  Kamera katika sehemu ya kuandikia.
 2. Piga picha mpya au video, ama chagua picha au video iliyopo kwenye kichaguzi.
 3. Chagua unachotaka kuongeza kwenye picha au video.
Kuongeza vibandiko au emoji
 1. Gusa
  Kibandiko > Kibandiko au Emoji.
 2. Gusa kipengee ambacho ungependa kutumia.
  • Ili usogeze kipengee, kiguse na ukishikilie, kisha kiburute.
  • Ili ubadilishe ukubwa wa kipengee, kifinye au kipanue ili kiwe kidogo au kikubwa.
  • Ili kuzungusha kipengee, kifinye na ukigeuze.
Kuongeza maandishi
 1. Gusa Maandishi
  katika sehemu ya juu ya skrini.
 2. Andika unachotaka katika sehemu ya maandishi.
  • Ili uchague rangi, telezesha kidole chako juu na chini kwenye kiteua rangi.
  • Ili uchague aina ya fonti, gusa Maandishi
   kwa kurudia. Gusa skrini ili uthibitishe aina ya fonti.
  • Ili ubadilishe ukubwa wa maandishi, yafinye au yapanue ili yawe madogo au makubwa.
  • Ili uzungushe maandishi, finya na ugeuze maandishi.
Kuchora
 1. Gusa
  Chora katika sehemu ya juu ya skrini.
 2. Tumia kidole chako kuchora unachotaka.
  • Ili uchague rangi, telezesha kidole chako juu na chini kwenye kiteua rangi. Unaweza kuchagua rangi ya kila mstari unaouchora.
Kutumia vichujio
 1. Telezesha kidole juu kwenye picha au video.
 2. Chagua kichujio.
Kunyamazisha sauti ya video
 1. Gusa
  Nyamazisha ili uondoe sauti kwenye video yako.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La