Jinsi ya kuhariri picha na video

Android
iPhone
Wavuti na Kompyuta ya dawati
WhatsApp inakuruhusu kuweka picha na video zako jinsi unavyopenda kwa kuongeza vibandiko, emoji, maandishi, michoro na vichujio.
Kuhariri picha na video
Kupiga picha au kurekodi video mpya
  1. Gusa Ambatisha
    > Kamera
    katika sehemu ya maandishi.
  2. Gusa Video au Picha, kisha urekodi video mpya au upige picha mpya.
  3. Kuanza kuhariri picha au video yako.
Kutumia picha au video iliyopo
  1. Gusa Ambatisha
    > Matunzio
    katika sehemu ya maandishi.
  2. Chagua picha au video.
  3. Kuanza kuhariri picha au video yako.
Kukata au kuzungusha picha yako
  1. Gusa
    .
    • Ili ukate picha yako, gusa na ushikilie kitambulishi chochote, kisha ukiburute ndani au nje hadi ukubwa unaotaka.
    • Ili uzungushe picha, gusa Zungusha
      mara kwa mara.
  2. Gusa Nimemaliza unapomaliza.
Kutumia kichujio kwenye picha yako
  1. Telezesha kidole juu kwenye picha.
  2. Chagua kichujio.
  3. Gusa picha unapomaliza.
Kuweka vibandiko au emoji kwenye picha au video yako
  1. Gusa
    > Vibandiko au Emoji.
  2. Gusa kipengee ambacho ungependa kutumia.
    • Ili usogeze kipengee, kiguse na ukishikilie, kisha kiburute.
    • Ili ubadilishe ukubwa wa kipengee, kifinye au kipanue ili kiwe kidogo au kikubwa.
    • Ili kuzungusha kipengee, kibane na ukigeuze.
  3. Gusa sehemu yoyote kwenye picha yako unapomaliza.
  4. Ili ufute emoji au kibandiko, kiburute kwenye Tupio
    linaloonekana.
Kuweka maandishi kwenye picha au video yako
  1. Gusa Maandishi
    yaliyo juu ya skrini.
  2. Andika maandishi unayotaka katika kisanduku cha maandishi.
  3. Gusa Nimemaliza unapomaliza.
Kubadilisha mwonekano wa maandishi yako
  1. Gusa kisanduku cha maandishi.
    • Ili ubadilishe rangi ya maandishi na utelezeshe kidole chako juu na chini kwenye Kiteua rangi.
    • Ili ubadilishe aina ya fonti, gusa
      mara kwa mara. Fonti hubadilika kila wakati. Gusa skrini ili uthibitishe aina mpya ya fonti.
    • Ili ubadilishe ukubwa wa maandishi, yabane au uyapanue ili kuyafanya madogo au makubwa.
    • Ili uzungushe maandishi, bana na ugeuze kisanduku maandishi.
    • Ili usogeze kisanduku cha maandishi, kiburute kwenye eneo jipya.
  2. Gusa sehemu yoyote kwenye skrini unapomaliza.
  3. Kumbuka: Unaweza pia kuchagua fonti na rangi kabla ya kuweka maandishi yako.
Kuchora kwenye picha au video yako
  1. Gusa
    .
  2. Chagua rangi na unene wa kalamu.
    • Ili ubadilishe rangi ya kalamu, telezesha kidole chako juu na chini kwenye Kiteua rangi.
    • Unaweza kubadilisha unene wa kalamu kwa kugusa moja ya aikoni
      iliyo chini ya picha yako.
  3. Tumia kidole chako kuchora unachotaka.
    • Ili ufute mstari unapofuta, gusa Tengua
      .
  4. Gusa Nimemaliza unapomaliza.
Kutia ukungu picha yote au sehemu ya picha
  1. Gusa
    .
  2. Gusa zana ya Kutia Ukungu
    , iliyo chini ya picha yako.
  3. Tumia kidole chako kutia ukungu sehemu yoyote ya picha yako.
    • Gusa
      ili Kutengua madoido ya ukungu.
  4. Gusa Nimemaliza unapomaliza.
Kuzima video yako
  1. Gusa Zima
    ili uzime sauti kwenye video yako.
Kutuma maudhui yako
Ukimaliza kuhariri maudhui yako, gusa Tuma
.
Rasilimali zinazohusiana
Jinsi ya kutuma maudhui kwenye Android
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La