Kuongeza na kuondoa washiriki wa kikundi

Unaweza kuongeza au kuwaondoa washiriki kwenye kikundi ikiwa wewe ndiwe msimamizi wa kikundi.
Kuongeza washiriki
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp.
 2. Bofya mada ya kikundi.
  • Au, bofya Menyu (
   au
   ) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
 3. Bofya Ongeza mshiriki
  .
 4. Tafuta au chagua mwasiliani wa kuongeza kwenye kikundi.
 5. Bofya tiki ya kijani
  .
 6. Bofya ONGEZA MSHIRIKI.
Kuondoa washiriki
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp.
 2. Bofya mada ya kikundi.
  • Au, bofya Menyu (
   au
   ) kwenye kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
 3. Fanya kiashiria kuelee juu ya jina la mshiriki unayetaka kumwondoa, kisha bofya Menyu
  .
 4. Bofya Ondoa > ONDOA.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La