Jinsi ya kudhibiti arifa zako

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Mapendeleo ya arifa yanaweza kudhibitiwa kwenye mipangilio ya WhatsApp.

Kubadili mipangilio ya arifa za WhatsApp
Fungua WhatsApp > gusa Chaguo zaidi
> Mipangilio > Arifa.
Unaweza kubadilisha arifa za ujumbe, vikundi na simu kwa kuchagua:
  • Iwapo unataka kuwasha au kuzima milio kwa ujumbe unaoingia na unaotumwa.
  • Mlio au toni ya arifa.
  • Muda wa mtikisiko.
  • Iwapo unataka kuonyesha arifa ibukizi kwenye vifaa vya Android 9 na matoleo ya zamani. Hatua hii huruhusu arifa kuonekana katikati ya skrini yako.
  • Rangi ya mwanga wa arifa kwa simu zinazoruhusu kubadilisha.
  • Iwapo utatumia arifa za kipaumbele cha juu kwenye Android 5 na matoleo mapya zaidi. Hatua hii huonyesha muhtasari wa arifa juu ya skrini yako na inaweza kutumika kuzima arifa za kuchungulia.
Kumbuka: Kuzima arifa za kipaumbele cha juu kutasababisha arifa za WhatsApp zionyeshwe katika sehemu ya chini kwenye skrini yako.
Ili uweke upya mipangilio ya arifa, gusa Mipangilio > Arifa > gusa Chaguo zaidi
> Weka upya mipangilio > WEKA UPYA.
Kuweka arifa upendavyo
Unaweza kuweka arifa upendavyo kwa kuteua chaguo tofauti za mlio, mtetemo, arifa ibukizi na mwanga:
  1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
  2. Gusa jina la mtu binafsi au soga ya kikundi.
  3. Gusa Arifa maalum > wekea alama Tumia arifa maalum.
Kumbuka: Simu za kikundi hutumia mlio chaguomsingi wa simu. Mlio huu wa simu hauwezi kuwekewa mapendeleo.
Kuzima arifa
  1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
  2. Gusa jina la mtu binafsi au soga ya kikundi.
  3. Gusa Zima arifa.
  4. Chagua kipindi cha muda ambao ungependa kuzima arifa kisha uguse SAWA.
Au, ondoa alama ya tiki kwenye Onyesha arifa ili uzuie arifa zisionekane.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kuzima au kuwasha arifa: iPhone | Web na Desktop | KaiOS
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La