Jinsi ya kudhibiti arifa zako

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows

Unaweza kudhibiti mapendeleo ya arifa kwenye mipangilio ya WhatsApp.
Fungua WhatsApp Web au WhatsApp Desktop > bofya Menyu (
au
) > Mipangilio > Arifa
.
Hapa unaweza kufanya mabadiliko kwenye:
 • Sauti
 • Arifa za Eneokazi
 • Mwonekano wa Muhtasari
Pia unaweza kuzima arifa zote za soga na sauti kwa muda fulani maalum. Kuwasha arifa tena, bofya Arifa na sauti zimezimwa.Bofya kurejesha. (
au
).
Kunyamazisha soga za binafsi au za kikundi
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Bofya Menyu
  > Nyamazisha arifa.
 3. Chagua muda:
  • Saa 8
  • Wiki 1
  • Kila wakati
 4. Bofya NYAMAZISHA ARIFA.
Kuwasha arifa tena, tafuta soga zilizonyamazishwa, bofya Menyu
> Ruhusu arifa.
Kumbuka: Ukinyamazisha soga ya kikundi au ya binafsi kwenye simu yako, pia itanyamazishwa kwenye WhatsApp Web na Desktop. Mipangilio mingine yote ya arifa iliyo kwenye simu na kompyuta yako haiathiriani.
Kuzima arifa zote
Ili uzime arifa zote, ikiwa ni pamoja na simu zinazoingia, funga WhatsApp Web au WhatsApp Desktop. Ili uwashe arifa zinazotokea kwenye eneokazi, fungua WhatsApp.
Au, unaweza kuwezesha Usisumbue kwenye Mac au Focus Assist kwenye Windows. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuzima arifa, tafadhali tembelea tovuti ya Msaada wa Apple au tovuti ya Msaada wa Microsoft.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La