Kuhusu kuunda jina la biashara

Jina la biashara lazima liwakilishe biashara au shirika.
Kanuni za kuunda jina la biashara
Ili utimize vigezo vya kuwa na “Akaunti rasmi ya biashara", majina ya biashara hayawezi kuwa na:
  • Herufi zote kubwa, isipokuwa vifupisho. Herufi ya kwanza tu ndiyo inaweza kuwa kubwa. Viunganishi havitakiwi kuwa katika herufi kubwa. Kwa mfano:
    • Sahihi: Vitafunio Vitamu au Vileja na Mapochopocho ya Asha
    • Si Sahihi: VITAFUNIO VITAMU* au Vileja Na Mapochopocho ya Asha
  • Nafasi yoyote ya ziada kati ya maneno. Majina ya biashara lazima yatumie uandishi wa kuacha nafasi moja.
  • Uakifishaji usiohitajika
  • Emoji
  • Ishara (mfano: ®)
  • Mfululizo wa herufi zisizo za alfabeti na tarakimu (maandishi ambayo si nambari wala za herufi)
  • Herufi zozote hizi maalum: ~!@#$%^&*()_+:;"'{}[]\|<>,/?
Kumbuka: Mwongozo huu wa muundo wa maandishi hautumiki kwa biashara ambazo tayari chapa zao ziko hivyo kwa nje. Katika hali hiyo, jina la biashara linalotumika kwenye programu ya WhatsApp Business linaweza kuwa na uakifishi, herufi kubwa, n.k. inavyolingana na chapa ya nje.
Pia, majina ya biashara hayawezi kuwa na:
  • Jina kamili la mtu
  • Neno la kawaida (mfano: Mtindo)
  • Eneo la kawaida la kijiografia (mfano: New York)
  • Herufi tatu au chache zaidi
Hatimaye, majina ya biashara hayawezi kuwa na mfano wowote wa neno "WhatsApp". Pata maelezo zaidi kwa kutembelea Miongozo yetu ya Chapa.
Kumbuka: Ikiwa akaunti yako ya biashara imeorodheshwa kama "Akaunti rasmi ya biashara", kubadilisha jina lako la biashara kunaweza kusababisha akaunti yako kupoteza hadhi yake ya "Akaunti rasmi ya biashara".
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La