Jinsi ya kubadilisha lugha ya WhatsApp

WhatsApp inapatikana kwa zaidi ya lugha 40 kwenye iPhone na hadi 60 kwenye Android. WhatsApp hufuata lugha unayotumia kwenye simu yako. Kwa mfano, ikiwa utabadilisha lugha ya simu yako kuwa Kihispania, WhatsApp itakuwa katika Kihispania.
Kubadilisha lugha ya simu yako
  • Android: Nenda kwenye Mipangilio ya simu yako > Udhibiti wa jumla > Lugha. Gusa na ushikilie lugha ili uisogeze juu au uguse
    .
  • iPhone: Nenda kwenye
    > Jumla > Lugha na Eneo> Lugha ya iPhone. Gusa na ushikilie lugha ili uisogeze juu au uguse Weka Lugha.
  • KaiOS: Bonyeza Mipangilio kwenye menyu ya programu > sogeza kando ili uchague Kuweka mapendeleo > sogeza chini kisha ubonyeze Lugha > bonyeza Lugha > chagua lugha ambayo ungependa kuitumia > bonyeza SAWA au CHAGUA.
Chaguo inayopatikana katika baadhi ya nchi
Ikiwa unatumia simu ya Android, unaweza kuwa na chaguo ya kubadili lugha ya WhatsApp kwenye programu. Unaweza kuchagua lugha yako kwenye Skrini ya mwanzo unapoanza kutumia WhatsApp au ikiwa tayari unatumia WhatsApp:
  1. Gusa
    > Mipangilio > Soga > Lugha ya Programu.
  2. Chagua lugha ambayo ungependa.
Ikiwa huoni chaguo hizi, labda hazipatikani kwenye nchi uliyopo.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La