Â
Jinsi ya kubadilisha lugha ya WhatsApp
WhatsApp inapatikana kwa zaidi ya lugha 40 kwenye iPhone na hadi 60 kwenye Android. WhatsApp hufuata lugha unayotumia kwenye simu yako. Kwa mfano, ukibadilisha lugha ya simu yako kuwa Kihispania, WhatsApp itakuwa katika Kihispania.
Kubadilisha lugha ya simu yako
- Android: Nenda kwenye simu yako Mipangilio > Mfumo > Lugha na uingizaji data > Lugha. Gusa na ushikilie lugha ili usogeze juu, au gusa Ongeza lugha.
- iPhone: Nenda kwenye Mipangilio> Jumla > Lugha na Eneo > Lugha ya iPhone. Chagua lugha, kisha gusa Badilisha kuwa {language}.
- KaiOS: Bonyeza Mipangilio kwenye menyu ya programu > sogeza hadi kando ili kuchagua Kuweka mapendeleo > sogeza chini kisha bonyeza Lugha > bonyeza Lugha > chagua lugha unayotaka kutumia > bonyeza SAWA au CHAGUA.
Chaguo linalopatikana katika baadhi ya nchi
Ikiwa unatumia simu ya Android, unaweza kuwa na chaguo la kubadili lugha ya WhatsApp kutoka kwenye programu. Moja ya chaguo ni kuchagua lugha unayotaka kwenye skrini ya mwanzo ya Karibu. Au, ikiwa tayari unatumia WhatsApp:
- Fungua WhatsApp.
- Gusa Chaguo zaidi> Mipangilio > Soga > Lugha ya Programu.
- Chagua lugha unayotaka.
Ikiwa huoni machaguo haya, labda hayapatikani katika nchi yako.