Jinsi ya kutuma ujumbe wa sauti
Ujumbe wa sauti kwenye WhatsApp hukuruhusu kuwasiliana papo hapo na waasiliani na vikundi. Unaweza kuutumia kuwasilisha taarifa muhimu na za haraka. Kwa hivyo, ujumbe wote wa sauti hupakuliwa kiotomatiki.
Kutuma ujumbe wa sauti
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Bofya maikrofoni na uanze kuzungumza.
- Mara ukimaliza, bofya alama ya tiki .
- Wakati unarekodi ujumbe wa sauti, unaweza kubofya aikoni ya X ili ughairi.
Kwenye ujumbe wa sauti uliotumwa utaona:
- Maikrofoni ya kijivu kwenye ujumbe wa sauti ambao mpokeaji wako hajaucheza.
- Maikrofoni ya bluu kwenye ujumbe wa sauti ambao mpokeaji wako ameucheza.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kucheza ujumbe wa sauti