Kuhusu upeo wa kusambaza

Unaweza kusambaza ujumbe kwenye hadi soga tano kwa wakati mmoja. Ikiwa ujumbe tayari umesambazwa, unaweza kuusambaza kwenye hadi soga tano, ikiwa ni pamoja na kwenye kikundi kimoja.
Hata hivyo, ujumbe ukisambazwa kupitia msururu wa soga tano au zaidi, ikiwa ina maana kwamba umesambazwa angalau mara tano tangu mtumaji wa kwanza, aikoni ya vishale viwili
iliyo na maandishi "Umesambazwa mara nyingi" itaonyeshwa. Ujumbe kama huo unaweza tu kusambazwa kwenye soga moja kwa wakati mmoja, kama njia ya kusaidia kuweka mazungumzo kwenye WhatsApp kuwa ya karibu na ya binafsi. Kufanya hivyo pia husaidia kupunguza kasi ya uvumi, ujumbe unaozagaa na habari bandia.
Ujumbe uliosambazwa hufumbwa mwisho hadi mwisho
Ujumbe uliosambazwa una mfumo wa kuhesabu unaofuatilia ni mara ngapi ujumbe umesambazwa. Kwa faragha yako, WhatsApp haijui ni mara ngapi ujumbe umesambazwa na haiwezi kuona maudhui ya ujumbe wako wowote kwenye soga zilizofumbwa mwisho kwa mwisho. Pata maelezo zaidi kuhusu ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwenye makala haya.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kusambaza ujumbe kwenye: Android | iPhone | Web na Desktop | KaiOS
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La