Kuhusu kutumia programu ya WhatsApp Business kuwasiliana na wateja wako

Tofauti na WhatsApp Messenger, ambayo imeundwa kwa ajili ya mawasiliano ya binafsi, programu ya WhatsApp Business imeundwa kwa ajili ya mawasiliano ya nje ya biashara. Kila programu inatii GDPR kulingana na madhumuni yake yaliyokusudiwa. Ikiwa una biashara ndogo hadi ya kati, unapaswa kutumia programu ya WhatsApp Business kwa mawasiliano ya kibiashara na wateja wako. Unaweza kupakua programu ya WhatsApp Business bila malipo kutoka kwenye Duka la Google Play na App Store.
Kwa maelezo zaidi kuhusu GDPR na kudhibiti nambari zilizo kwenye kitabu cha anwani cha kifaa chako, soma makala haya.
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyotumia taarifa za biashara yako, soma sehemu ya Desturi Zetu za Data kwenye Masharti yetu ya Huduma ya WhatsApp Business.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La