Kuhusu kupiga soga na biashara

Ni rahisi kutofautisha kati ya akaunti ya kibinafsi na akaunti ya biashara kwenye WhatsApp. Kwenye soga, gusa jina la unayewasiliana naye ili uone jalada lake. Ikiwa ni biashara, jalada lake litakuwa na mojawapo ya lebo zifuatazo:
  • Akaunti rasmi ya biashara: WhatsApp imebaini kuwa biashara inayojulikana na halisi inamiliki akaunti hii. "Akaunti rasmi ya biashara" ina beji ya tiki ya kijani kwenye jalada lake na karibu na kijajuu katika orodha ya soga kati yako na biashara hiyo. Jina la biashara hiyo linaonekana hata ikiwa haujaongeza biashara hiyo kwenye kitabu chako cha anwani.
  • Akaunti ya biashara: Hii ndiyo hali chaguomsingi kwa biashara zinazofungua akaunti kwenye mojawapo ya bidhaa za WhatsApp Business.
Dokezo: "Akaunti rasmi ya biashara" haionyeshi kuwa WhatsApp inaidhinisha biashara hii.
Kwa nini ninaona ujumbe mpya wa mfumo kwenye soga zangu za WhatsApp?
Baadhi ya biashara unazowasiliana nazo kwa soga kwenye WhatsApp zinaweza kuchagua kutumia Facebook au kampuni nyingine kuzisaidia kudhibiti na kuhifadhi ujumbe wao.
Utaona ujumbe ufuatao, biashara inapochagua:
  • Kutumia mshirika: Utaona “Biashara hii hushirikiana na kampuni nyingine kushughulikia soga hii.”
  • Kutumia Huduma zinazopangishwa na Facebook:Utaona “Biashara hii hutumia huduma salama kutoka kampuni ya Facebook kushughulikia soga hii.”
Ikiwa biashara inadhibiti soga zake yenyewe, utaona: “Ujumbe na simu hufumbwa mwisho hadi mwisho. Hakuna yeyote nje ya soga hii, hata WhatsApp, anayeweza kusoma wala kuzisikiliza.”
Hata kama biashara itachagua kutumia Facebook kuweka ujumbe wake, Facebook haitatumia ujumbe wako kiotomatiki kuamua matangazo unayoyaona. Kama ilivyo kwenye njia nyinginezo za mawasiliano, kama vile vituo vya huduma kwa simu au barua pepe, biashara zinaweza kutumia mawasiliano na wateja kwa madhumuni yao ya uuzaji, ambayo yanaweza kujumuisha utangazaji kwenye Facebook au kwingineko. Unaweza kuwasiliana na biashara husika wakati wowote ili upate maelezo zaidi kuhusu desturi zake za faragha.
Ikiwa hutaki kupokea ujumbe kutoka kwa mtu au biashara, unaweza kumzuia moja kwa moja kwenye soga au umfute kutoka kwenye orodha yako ya anwani.
Salama na faragha wakati wote
Kila ujumbe wa WhatsApp hulindwa na itifaki ile ile ya ufumbaji wa Signal ambayo hudumisha usalama wa ujumbe kabla haujatoka kwenye kifaa chako. Unapotuma ujumbe kwenda kwenye akaunti ya biashara ya WhatsApp, ujumbe wako huwasilishwa kwa usalama kwenda sehemu iliyochaguliwa na biashara hiyo.
Rasilimali zinazohusiana
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La