Jinsi ya kuweka akaunti ya WhatsApp Business kwenye Ukurasa wa Facebook

Unapotumia programu ya WhatsApp Business, unaweza kuunganisha Ukurasa wako wa Facebook na akaunti yako ya WhatsApp Business.
Kidokezo cha Biashara: Kuunganisha akaunti yako ya WhatsApp Business kunawawezesha wateja wanaotembelea Ukurasa wako wa Facebook kukutumia ujumbe moja kwa moja kwenye WhatsApp kwa kubofya mara moja tu.
Ili kuunganisha akaunti hizi na kuwezesha usawazishaji, lazima uwe na yafuatayo:
 • Ukurasa wa Facebook kwa ajili ya biashara yako.
 • Akaunti kwenye programu ya WhatsApp Business.
 • Matoleo ya hivi karibuni ya programu za vifaa vya mkononi.
Kuunganisha akaunti yako ya WhatsApp Business na Ukurasa wa Facebook
Unaweza kuunganisha akaunti zako kutoka kwenye programu ya WhatsApp Business.
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Kwenye Android, gusa Chaguo zaidi. Kwenye iPhone, gusa Mipangilio.
 3. Gusa Zana za Biashara > Facebook na Instagram.
 4. Gusa Facebook > ENDELEA. Itafungua ukurasa wa kuingia kwenye Facebook.
 5. Weka maelezo ya kuingilia kwenye akaunti yako ya Facebook. Gusa Ingia.
 6. Chagua Ukurasa wa Facebook unaotaka kuunganisha na akaunti yako ya WhatsApp Business. Gusa Unganisha WhatsApp. .
  • Ikiwa huna ukurasa wa Facebook, utapewa chaguo la kufungua.
Sasa utaona Kitufe cha WhatsApp kwenye ukurasa wako wa Facebook.
Mara unaporudi kwenye programu ya WhatsApp Business, utaona ukurasa wako wa Facebook uliounganishwa upande wa juu ya skrini ya Facebook na Instagram.
Kusawazisha taarifa zako za biashara kwenye Facebook na WhatsApp
Unaposawazisha akaunti zako, mabadiliko yoyote unayofanya kwenye taarifa za biashara katika ukurasa wako wa Facebook zitaonekana kiotomatiki kwenye jalada lako la WhatsApp Business.
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Kwenye Android, gusa Chaguo zaidi. Kwenye iPhone, gusa Mipangilio.
 3. Gusa Zana za Biashara > Facebook na Instagram.
 4. Gusa Akaunti ya Facebook unayotaka kusawazisha na programu ya WhatsApp Business.
 5. Washa Sawazisha jalada na Ukurasa > Ruhusu. Kwenye iPhone, washa Sawazisha jalada na ukurasa.
Usawazishaji huu unafanya kazi kuelekea upande mmoja tu, kutoka kwenye Ukurasa wako wa Facebook kwenda kwenye programu ya WhatsApp Business. Kwa mfano: ukijaribu kubadilisha saa za biashara kwenye programu ya WhatsApp Business, utapata ujumbe wa onyo kuwa usawazishaji utakomeshwa. Ukiendelea kuhariri saa zako za kazi, akaunti yako ya WhatsApp Business itaonyesha saa mpya na Ukurasa wako wa Facebook utaonyesha saa za zamani.
Kumbuka: Mara tu usawazishaji unapoanzishwa, utafanya kazi kwenye wavuti na simu.
Kuondoa akaunti yako ya Facebook iliyounganishwa kwenye programu ya WhatsApp Business
Ikiwa hutaki tena akaunti zako ziwe zimeunganishwa, unaweza kutenganisha akaunti yako ya Facebook na WhatsApp kutoka kwenye programu ya WhatsApp Business.
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Kwenye Android, gusa Chaguo zaidi. Kwenye iPhone, gusa Mipangilio.
 3. Gusa Zana za Biashara > Facebook na Instagram.
 4. Gusa akaunti yako ya Facebook iliyounganishwa > Ondoa WhatsApp > ONDOA.
Mara baada ya kuondoa akaunti yako, haitaonekana tena kwenye skrini ya Facebook na Instagram.
Rasilimali zinazohusiana
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La