Kuhusu umri wa chini wa kutumia WhatsApp

Ni lazima uwe na angalau umri wa miaka 13 (au umri mkubwa zaidi unaohitajika katika nchi uliko) ili ujisajili na utumie WhatsApp.
Tafadhali rejelea Masharti yetu ya Huduma kwa maelezo zaidi.
Dokezo:
  • Kuunda akaunti ukitumia taarifa za uongo ni ukiukaji wa Masharti yetu.
  • Kusajili akaunti kwa niaba ya mtu aliye chini ya umri pia ni ukiukaji wa Masharti yetu.
Kuwaweka watumiaji salama
Tunatoa zana, vipengele na nyenzo mbalimbali ili kuwaweka watumiaji salama. Kwa mfano, tunahakikisha kuwa watu hawawezi kutafuta namba yako ya simu kwenye WhatsApp na mtumiaji anaweza:
  • Kuchagua anayeweza kuwasiliana nawe
  • Kudhibiti ni nani anayeweza kukuongeza kwenye soga za kikundi
  • Kuficha maelezo yako ya binafsi kama vile maelezo yako ya mara ya mwisho kuonwa na kuwa mtandaoni, picha ya jalada na kuhusu
  • Kuondoka kwenye soga za kikundi kimyakimya
Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu maelezo salama na ya faragha kwa ajili ya watumiaji vijana kwenye WhatsApp hapa.
Kuripoti mtoto aliye chini ya umri
Ikiwa mtoto wako aliye chini ya umri unaoruhusiwa alifungua akaunti ya WhatsApp, unaweza kumwonyesha jinsi ya kufuta akaunti yake. Unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya kufuta akaunti kwenye Kituo chetu cha Msaada.
Ikiwa ungependa kuripoti akaunti ya mtu aliye chini ya umri, tafadhali tutumie barua pepe. Kwenye barua pepe yako, tafadhali weka nyaraka zifuatazo na upunguze au ufiche taarifa zozote za binafsi zisizohusiana na ripoti unayopiga:
  • Uthibitisho wa umiliki wa namba ya WhatsApp (kwa mfano, nakala ya kitambulisho kilichotolewa na serikali na bili ya simu iliyo na jina lilo hilo)
  • Uthibitisho wa kuwa na mamlaka ya mzazi (kwa mfano, nakala ya cheti cha kuzaliwa au kuasiliwa kwa mtoto mwenye umri wa chini)
  • Uthibitisho wa tarehe ya kuzaliwa kwa mtoto (kwa mfano, nakala ya cheti cha kuzaliwa au kuasiliwa kwa mtoto mwenye umri wa chini)
Tutafunga akaunti hiyo ya WhatsApp haraka ikiwa itathibitishwa kuwa akaunti hiyo ni ya mtoto aliye na umri wa chini. Hutapokea uthibitisho wa hatua hii. Uwezo wetu wa kukagua na kuchukua hatua stahiki kutokana na ripoti unaboreshwa sana na ukamilifu wa maelezo tuliyoomba hapo juu.
Ikiwa akaunti ya mtoto iliyoripotiwa haijathibitishwa kwa usahihi kuwa inamilikiwa na mtoto mwenye umri wa chini, basi hatuwezi kuichukulia akaunti hiyo hatua. Katika hali hii, ikiwa wewe si mzazi wa mtoto huyu, basi tunapendekeza sana umhimize mzazi uwasiliane nasi kwa kutumia maelekezo yaliyo hapo juu.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La