Â
Kuhusu umri wa chini wa kutumia WhatsApp
Kama unaishi katika nchi iliyo kwenye Eneo la Uchumi la Ulaya (ambalo linajumuisha Jumuiya ya Ulaya), na nchi yoyote iliyojumuishwa au eneo (kwa pamoja inayojulikana kama Eneo la Ulaya), ni sharti uwe na angalau umri wa miaka 16 (au umri mkubwa zaidi unaohitajika nchini kwako) ili kujisajili na kutumia WhatsApp.
Ikiwa unaishi katika nchi nyingine yoyote isipokuwa zile zilizo katika Eneo la Ulaya, lazima uwe na umri wa angalau miaka 13 (au umri mkubwa unaohitajika katika nchi yako) ili ujisajili na kutumia WhatsApp.
Tafadhali rejelea Masharti yetu ya Huduma kwa maelezo zaidi.
Kumbuka:
- Kuunda akaunti ukitumia taarifa za uongo ni ukiukaji wa Masharti yetu.
- Kusajili akaunti kwa niaba ya mtu aliye chini ya umri pia ni ukiukaji wa Masharti yetu.
Kuripoti mtoto aliye chini ya umri
Ikiwa mtoto wako aliye chini ya umri unaoruhusiwa alifungua akaunti ya WhatsApp, unaweza kumwonyesha jinsi ya kufuta akaunti yake. Unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya kufuta akaunti kwenye Kituo chetu cha Msaada.
Ikiwa ungependa kuripoti akaunti ya mtu aliye chini ya umri, tafadhali tutumie barua pepe. Kwenye barua pepe yako, tafadhali weka nyaraka zifuatazo na upunguze au ufiche taarifa zozote za binafsi zisizohusiana na ripoti unayopiga:
- Uthibitisho wa umiliki wa namba ya WhatsApp (kwa mfano, nakala ya kitambulisho kilichotolewa na serikali na bili ya simu iliyo na jina lilo hilo)
- Uthibitisho wa kuwa na mamlaka ya mzazi (kwa mfano, nakala ya cheti cha kuzaliwa au kuasiliwa kwa mtoto mwenye umri wa chini)
- Uthibitisho wa tarehe ya kuzaliwa kwa mtoto (kwa mfano, nakala ya cheti cha kuzaliwa au kuasiliwa kwa mtoto mwenye umri wa chini)
Tutafunga akaunti hiyo ya WhatsApp haraka ikiwa itathibitishwa kuwa akaunti hiyo ni ya mtoto aliye na umri wa chini. Hutapokea uthibitisho wa hatua hii. Uwezo wetu wa kukagua na kuchukua hatua stahiki kutokana na ripoti unaboreshwa sana na ukamilifu wa maelezo tuliyoomba hapo juu.
Ikiwa akaunti ya mtoto iliyoripotiwa haijathibitishwa kwa usahihi kuwa inamilikiwa na mtoto mwenye umri wa chini, basi hatuwezi kuichukulia akaunti hiyo hatua. Katika hali hii, ikiwa wewe si mzazi wa mtoto huyu, basi tunapendekeza sana umhimize mzazi uwasiliane nasi kwa kutumia maelekezo yaliyo hapo juu.