Jinsi ya kupiga simu ya video ya kikundi

Android
iPhone
Simu ya kikundi huruhusu washiriki kupigiana simu za video kwa kutumia WhatsApp. Unapopokea simu ya video ya kikundi, skrini ya simu ya video ya kikundi cha WhatsApp inayoingia itaonyesha washiriki waliopo kwenye simu hiyo, mtu wa kwanza kwenye orodha ndiye mshiriki aliyekuongeza. Historia ya simu ya video ya kikundi itaonekana kwenye kichupo cha SIMU. Unaweza kugusa historia ya simu ili uone washiriki mahususi kwenye simu hiyo. Unaweza pia kujiunga na simu ambazo hukujibu iwapo bado zinaendelea.
Kupiga simu ya video ya kikundi
Kupiga simu ya video ya kikundi kutoka kwenye soga ya kikundi
  1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp unachotaka kupigia simu ya video.
  2. Ikiwa kikundi chako cha soga kina washiriki 32 au wachache, gusa Simu ya video
    kisha uthibitishe uamuzi wako.
  3. Kumbuka: Ikiwa kuna zaidi ya washiriki 32, gusa Simu ya kikundi
    kisha uchague hadi washiriki 32 ili wajiunge na simu yako ya video. Kisha gusa Simu ya video
    .
Kupiga simu ya video ya kikundi kutoka kwenye kichupo cha SIMU
  1. Fungua WhatsApp, kisha gusa kichupo cha SIMU.
  2. Gusa Simu mpya
    > Simu mpya ya kikundi.
  3. Tafuta washiriki unaotaka kuwaongeza kwenye simu, kisha gusa Simu ya video
    .
Kupiga simu ya video ya kikundi kutoka kwenye soga ya binafsi
  1. Fungua soga ya WhatsApp ya mmoja wa watu unaotaka kuwapigia simu ya video.
  2. Gusa Simu ya video
    .
  3. Mara baada ya mshiriki kukubali simu, gusa Fungua
    > Ongeza mshiriki.
  4. Tafuta mshiriki mwingine unayetaka kumwongeza kwenye simu kisha gusa ONGEZA.
  5. Gusa Ongeza mshiriki kama unataka kuongeza washiriki zaidi.
Kujiunga na simu ya video ya kikundi
Kujiunga na simu ya video ya kikundi inayoingia
  1. Utapokea arifa mtu anapokualika ujiunge na simu ya video ya kikundi.
  2. Ili ufungue skrini ya maelezo ya simu, gusa Jiunge.
    Kumbuka: Ikiwa bado hauko tayari kujiunga, gusa Puuza.
  3. Kutoka kwenye skrini ya maelezo ya simu, unaweza kukagua kwanza washiriki wa simu na waalikwa wengine.
  4. Gusa Jiunge ili ujiunge kwenye simu.
  5. Ukiwa kwenye simu, gusa Fungua
    ili ufungue skrini ya maelezo ya simu.
    • Gusa Ongeza mshiriki ili uongeze washiriki zaidi kwenye simu.
    • Gusa PIGA ili utume arifa kwa watu ambao wameshaalikwa.
Kujiunga na simu ya video ya kikundi uliyokosa kupitia kichupo cha SIMU
  1. Ikiwa simu inaendelea, gusa simu ambayo ungependa kujiunga nayo. Hatua hii itafungua skrini ya maelezo ya simu.
  2. Kwenye menyu ya simu, gusa Jiunge.
Kujiunga na simu ya video ya kikundi uliyokosa kupitia soga ya kikundi
Ikiwa simu ilianzishwa kutoka kwenye soga ya kikundi, unaweza kujiunga kwa kufungua soga hiyo kisha uguse Jiunge.
Kunyamazisha mtu mwengine
Unaweza kunyamazisha washiriki wengine kwenye simu ya kikundi. Ili ufanye hivyo, gusa na ushikilie jina la mshiriki. Kisha bonyeza Nyamazisha. Mshiriki anaweza kujiwashia maikrofoni wakati wowote kwa kugusa aikoni ya maikrofoni. Unaweza kumtumia ujumbe mshiriki moja kwa moja kwenye simu ya kikundi kwa kugusa na kushikilia kigae chake.
Kumbuka:
  • Ni washiriki 8 tu ndio wanaweza kuwa katika simu ya video kwa wakati mmoja.
  • Hakikisha kwamba wewe na unaowasiliana nao mna muunganisho imara wa intaneti wakati wa kupiga au kupokea simu za video. Ubora wa simu ya video utategemea mtu mwenye muunganisho hafifu zaidi.
  • Wakati wa simu ya video ya kikundi, unaweza kuzima video yako kwa kugusa Zima video
    .
  • Huwezi kuondoa mshiriki wakati mko kwenye simu ya video ya kikundi. Mtumiaji atahitaji kukata simu ili kujiondoa kwenye simu hiyo.
  • Unaweza kuwa kwenye simu ya video ya kikundi na mtu ambaye umemzuia. Hata hivyo, huwezi kumwongeza mtu ambaye umemzuia au mtu ambaye amekuzuia kwenye simu.
  • Upigaji wa simu ya video unapatikana tu kwenye simu za Android zinazotumia toleo la 4.1 au matoleo mapya.
Rasilimali zinazohusiana:
  • Jinsi ya kupiga simu ya video kwenye: Android | iPhone
  • Jinsi ya kupiga simu ya video ya kikundi kwenye iPhone
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La