Jinsi ya kunyamazisha au kuruhusu arifa za kikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kunyamazisha arifa za soga za kikundi kwa muda fulani. Bado utapokea ujumbe uliotumwa kwenye soga ya kikundi, lakini simu yako haitatetema au kutoa sauti ujumbe unapopokelewa.
Kunyamazisha arifa za kikundi
 1. Fungua WhatsApp > nenda kwenye soga ya kikundi > kisha bofya mada ya kikundi.
 2. Weka tiki kwenye kisanduku cha Nyamazisha.
 3. Chagua muda ambao ungependa kunyamazisha arifa.
 4. Bofya NYAMAZISHA ARIFA.
Au:
 • Kwenye orodha ya Soga zako, fanya kielekezi kielee juu ya kikundi kisha ubofye Menyu
  > Nyamazisha arifa. Chagua muda unaotaka kunyamazisha arifa > bofya NYAMAZISHA ARIFA.
 • Fungua soga ya kikundi, kisha bofya Menyu
  > Nyamazisha arifa. Chagua muda unaotaka kunyamazisha arifa > bofya NYAMAZISHA ARIFA.
Kurejesha arifa za kikundi
 1. Fungua WhatsApp > nenda kwenye soga ya kikundi > kisha bofya mada ya kikundi.
 2. Toa alama ya tiki kwenye sanduku la Imenyamazishwa.
 3. Bofya REJESHA.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La