Jinsi ya kuzima au kuwasha arifa kwenye kikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Mac
Unaweza kuzima arifa kwenye kikundi kwa muda maalumu. Bado utapokea ujumbe utakaotumwa kwenye soga ya kikundi, lakini simu yako haitatetema au kutoa sauti ujumbe unapopokelewa.
Kuzima arifa kwenye kikundi
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp.
  2. Bonyeza Chaguo > Zima > Sawa.
  3. Chagua muda ambao ungependa kuzima arifa.
  4. Bonyeza Sawa.
Au fungua soga husika ya kikundi. Bonyeza Chaguo > Maelezo ya Kikundi > Zima arifa. Chagua muda ambao ungependa kuzima arifa, kisha ubonyeze Sawa.
Kuwasha arifa kwenye kikundi
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp.
  2. Bonyeza Chaguo > Washa arifa > Sawa.
Au fungua soga husika ya kikundi. Bonyeza Chaguo > Maelezo ya Kikundi > Zima arifa > Hakuna.
Kumbuka: Unapozima arifa za ujumbe kwenye soga, kifaa chako hakitakuarifu kuhusu arifa zinapoingia. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kwamba:
  • Unaowasiliana nao hawataarifiwa kwamba umezima soga.
  • Bado unaowasiliana nao watapokea taarifa za kusomwa utakaposoma ujumbe wao.
  • Bado utakuwa na idadi ya ujumbe ambao hujausoma karibu na soga husika.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La