Jinsi ya kuzima au kuwasha arifa kwenye kikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Mac
Unaweza kuzima arifa kwenye kikundi kwa muda maalumu. Bado utapokea ujumbe utakaotumwa kwenye soga ya kikundi, lakini simu yako haitatetema au kutoa sauti ujumbe unapopokelewa.
Kuzima arifa kwenye kikundi
  1. Fungua soga ya kikundi.
  2. Gusa jina la soga husika ya kikundi.
  3. Gusa Zima arifa.
  4. Chagua muda ambao ungependa kuzima arifa, kisha uguse Sawa.
Gusa Zima arifa tena ili uwashe arifa za soga.
Kumbuka: Unapozima arifa za ujumbe kwenye soga, kifaa chako hakitakuarifu kuhusu arifa zinapoingia. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kwamba:
  • Unaowasiliana nao hawataarifiwa kwamba umezima soga.
  • Bado unaowasiliana nao watapokea taarifa za kusomwa utakaposoma ujumbe wao.
  • Bado utakuwa na idadi ya ujumbe ambao hujausoma karibu na soga husika.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La