Jinsi ya kutumia kusubiri simu

Android
iPhone
Ikiwa mtu anajaribu kukupiga simu kwenye WhatsApp wakati tayari upo kwenye simu ya sauti au video ya WhatsApp, utapokea arifa kulingana na aina ya simu na unaweza kuchagua kujibu au kukataa simu. Kufanya hivyo hakutaathiri simu inayoendelea.
Mtu akikupigia simu kwenye WhatsApp
Unaweza kuchagua kati ya zifuatazo:
  • Kata na Ukubali: Kata simu unayoendelea nayo sasa na upokee simu inayoingia.
  • Kataa: Kataa simu inayoingia na ubaki kwenye simu inayoendelea.
Mtu akikupigia simu nje ya WhatsApp
Ikiwa mtu anajaribu kukupigia simu kupitia simu ya mezani au ya rununu nje ya WhatsApp ukiwa kwenye simu ya WhatsApp ya sauti au ya video, unaweza kugusa:
  • Kata na Ukubali: Kata simu unayoendelea nayo sasa na upokee simu inayoingia.
  • Kataa: Kataa simu inayoingia na ubaki kwenye simu inayoendelea.
Kumbuka:
  • Kutegemea mtoa huduma wako, unaweza kutozwa gharama za simu zinazopigwa nje ya WhatsApp. Pia unaweza kutozwa kwa simu za sauti au video unazopiga kwa kutumia WhatsApp, ikiwa unatumia data ya mtandao wa ng'ambo au umezidi kipimo chako cha data.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La