Huwezi kubadilisha nambari ya simu

Kama una suala kutumia kipengele cha badilisha nambari, hakikisha kwamba:
  • Simu ya zamani uliyoingiza kwa sasa imesajiliwa kwenye akaunti yako ya WhatsApp. Unaweza kuona ni nambari ipi imesajiliwa kwa kwenda kwa WhatsApp Mipangilio, kisha gusa aikoni ya picha ya jalada lako. Kama nambari ya zamani ya simu haijasajiliwa, tafadhali isajili kwanza kabla ya kujaribu tena kubadilisha nambari ya simu yako.
  • Una SIM kadi amilifu na inayofanya kazi kwa nambari mpya ya simu unayotaka kuitumia kwa WhatsApp.
  • Una muunganisho thabiti wa selula..
  • Simu yako ina hifadhi ya ndani ya kutosha.
Ikiwa una masuala ya kusajili nambari yako mpya ya simu baada ya kubadilisha nambari ya simu, tafadhali soma zaidi kuhusu usajili kwenye Android au iPhone.
Dokezo: Kubadilisha nambari ya simu yako hakuwezeshwi kwenye KaiOS. Hata hivyo, unaweza kusajili nambari yako mpya ya simu kwenye WhatsApp kwa kupitia kwenye mchakato wa usajili. Maelezo yako ya akaunti ya zamani hayatahamishwa kwenda kwa nambari yako mpya ya simu na utapoteza soga zako za kibinafsi na za kikundi.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La