Jinsi ya kuthibitisha namba yako ya simu

Android
iPhone
KaiOS
Ni lazima uthibitishe namba yako ya simu ili uanze kutumia WhatsApp.
Ili kuthibitisha namba yako ya simu:
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Bonyeza Masharti na Sera ili usome Masharti ya Huduma na Sera yetu ya Faragha.
 3. Bonyeza Kubali ili ukubali Masharti yetu kisha uendelee.
 4. Bonyeza Chagua nchi.
 5. Tafuta au uchague nchi yako kisha ubonyeze CHAGUA NCHI.
 6. Weka namba yako ya simu.
 7. Bonyeza Inayofuata > Sawa ili upokee msimbo wa uthibitishaji kupitia SMS.
 8. Weka msimbo wenye tarakimu 6 ambao umetumiwa kupitia SMS.
  • Ikiwa hukupokea msimbo, unaweza kubonyeza Tuma SMS tena au Nipigie ili mfumo wetu wa kiotomatiki ukupigie simu ili ukupe msimbo.
 9. Weka jina lako. Tafadhali kumbuka:
  • Idadi ya juu ya herufi kwenye jina ni herufi 25.
  • Pia unaweza kuweka Picha ya jalada.
 10. Bonyeza Nimemaliza.
Kumbuka: Video hii inatumika kwa watumiaji wa WhatsApp wanaotumia JioPhone au JioPhone 2 pekee.

Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La