Jinsi ya kuthibitisha namba yako ya simu

Android
iPhone
KaiOS
WhatsApp inahitaji namba ya simu inayofanya kazi ili kuunda akaunti. Ikiwa unatatizika kuthibitisha, tafadhali hakikisha yafuatayo:
 • Una toleo la hivi karibuni la WhatsApp ulilosakinisha kutoka kwenye Duka la Programu.
 • Umeweka namba yako ya simu katika muundo kamili wa kimataifa, ikiwa na msimbo wa nchi (au chagua nchi yako kutoka kwenye orodha ya nchi).
  • Mfano wa namba ya simu ya Marekani ni: + 1 408-XX-XXXX.
 • Usijumuishe sifuri (0) zozote zinazotangulia au namba za kupiga nje ya nchi kwenye namba yako ya simu.
 • Simu yako inafikia intaneti yenye mawimbi thabiti kwa ukamilifu. Jaribu kufungua tovuti yoyote ili uhakikishe.
 • Simu yako inaweza kupokea ujumbe wa SMS za kimataifa.
 • Hutumii kifaa kisichoweza kutumika kama vile iPod touch au iPad.
 • Kifaa chako hakijafunguliwa kinyume na sheria.
 • Hakikisha unatumia namba ya simu inayoruhusiwa. Namba za simu zisizoruhusiwa haziwezi kusajiliwa kwenye WhatsApp, namba hizo ni pamoja na:
 • VoIP
 • Simu za mezani (Kumbuka: Simu za mezani zinakubaliwa tu kwenye programu ya WhatsApp Business)
 • Namba zisizolipiwa
 • Namba za kulipia unapopigia
 • Namba za ufikiaji wa jumla (UAN)
 • Namba za binafsi
Baada ya kuweka namba yako ya simu, tafadhali subiri SMS itumwe kwenye simu yako. SMS itakuwa na msimbo wa uthibitisho wa tarakimu 6, ambao unaweza kuuweka kwenye skrini ya uthibitisho katika WhatsApp. Msimbo wa uthibitisho ni wa kipekee na hubadilika kila unapothibitisha namba mpya ya simu au kifaa. Tafadhali usikisie msimbo wa uthibitisho kwani unaweza kufungiwa kwa muda.
Kumbuka: Ikiwa unatumia iCloud Keychain na umethibitisha namba hii hapo awali, unaweza kuthibitishwa kiotomatiki bila kupokea msimbo mpya kupitia SMS.
Ikiwa hukupokea msimbo wako kupitia SMS, mfumo wetu wa kiotomatiki unaweza kukupigia simu ili kukupatia msimbo wako. Tafadhali subiri muda wa dakika tano ukamilike na usihariri namba yako katika kipindi hicho. Baada ya dakika tano, gusa Nipigie.
Kumbuka: Kutegemea mtoa huduma wako, unaweza kutozwa gharama ya SMS na ya kupigiwa simu.
Ikiwa umefuata hatua hizi na huwezi kupokea msimbo, tafadhali fanya yafuatayo:
 1. Ondoa WhatsApp kwenye iPhone yako.
 2. Anzisha iPhone yako upya > zima iPhone yako na kisha uiwashe tena.
 3. Pakua toleo la hivi karibuni la WhatsApp kutoka kwenye Duka la Programu.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La